Posts

Showing posts from 2019

MVUA YASABABISHA UHARIBIFU WA MASHAMBA YA KAYA 93 RORYA MARA

Image
Na_Bazil Mjungu. ROYRA MARA : Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyo nyeesha Desemba 12/2019 katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilayani Rorya Mkoani Mara imesababisha maporomoko makubwa ya mawe na mmomonyoko mkubwa wa ardhi hali iliyopelekea kuharibika kwa mashamba ya Kaya zaidi ya 93. Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo (CCM) alitembelea eneo hilo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Charles Ochele na viongozi wengine wa Serikali za Vijiji na Kata kufika katika eneo la tukio na ujionea uharibifu mkubwa Mashamba kusombwa na Maji yenye Mawe Makubwa yaliyosababisha kutokea kwa mto na bonde kubwa huku za zaidi ekari 20 za mazao ya wananchi kusombwa na maji na kuharibiwa na mamia ya mawe yaliyoporomoka kutoka zaidi ya km 2 kutoka eneo la Mashamba n Mlima uliko. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Tatwe Mhe. Lameck Airo ametoa pole kwa wananchi na kuonyesha kusikitishwa na tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi na kuwashitua wananchi

ONA MADHARA YA KUMUAMSHA MDADA WA KAZI SAA 11 ALFAJIRI NA KUWAACHA BINTI ZAKO WAKILALA.

Image
Na Uhuru Kenyatta: Kumuamsha mdada wa kazi saa 11 alfajiri na kuwaacha binti zako wamelala Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mke Bora kuliko wanao.   Eti kumtumikisha dada wa kazi apige deki, apike, afue nguo, aoshe vyombo wakati wanao wanaangalia TV. Ni kumuandaa mdada wa kazi  kuwa mwanamke anayewajibika kuliko wanao. Kumuacha binti wa kazi aandae watoto kwenda shule, awaandalie uji mapema, awalishe, awasafishe wakati wanao wanacheza gemu kwenye simu au computer Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mama na mlezi bora kwa watoto kuliko wanao. Na kwakuwa yote hayo unayafanya kwa masimango na manyanyaso unamfanya mdada wa kazi kuwa jasiri mwenye kuzikabili changamoto za ndoa yake kuliko wanao. Ukimaliza kwa kusema mwanao akiwa hajui hayo yote, ndoa ikiharibika mnazunguka kutafuta maombi kwa wachungaji kumbe ninyi mmeharibu ndoa za watoto wenu. Msiwasumbue wachungaji. Rais Uhuru Kenyata. 🙏🙏🙏.

SIASA ZA IKUNGI NA HATIMA YA MAISHA YA WANAIKUNGI

Image
MAKALA YANGU: Ramadhani Ndoghwe: Jimbo la Singida Mashariki ni takribani miaka 9 limekuwa katika SIASA za UPOFU zisizokuwa na dhamira ya dhati kuwainua watu Kiuchumi na kijamii huduma za Afya na Maji zilikosekana kwa %70, Barabara hazikupitika, Vijana walikaririshwa kuwa maendeleo ni Kuku kuota Makucha  eti hayo ndio maendeleo wakasahau kuwa MTU NI AFYA, wakasahaulishwa Ukombozi FIKIRA CHANYA  na kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais John Pombe Magufuli za Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati. Mnamo September 2019 alipatikana Mbunge mwenyewe dahana halisi ya kuwasemea wananchi na kuleta chachu ya maendeleo katika Jimbo la Singida Mashariki na Vitu kama Miundombinu za Barbara, Maji na Afya zimeanza kutatulia na kuonyesha njia sahihi ya maana ya uongozi niseme Sasa tumetoka kule tulipokuwa na sasa tunaenda kutekeleza dhana hizo kikubwa ni kuamini kuwa TANZANIA ya Viwanda inawezekana Kwa sasa Jimbo la Singida Mashariki, Tumepata Mhe. Miraji Mtaturu kiongozi mwenye

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA GEITA MHE. VICKY KAMATA AMEUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA RAIS MAGUFULI ZA TANZANIA YA VIWANDA KWA KUKABIDHI VITU VYENYE THAMANI YA MILIONI 125. MKOANI GEITA.

Image
Na. Bazil Mjungu: Geita. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Mhe.Vicky Kamata ameunga mkono  juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa Tanzania ya Viwanda kwa kutoa Vyerehani 350 kwa Kata zote za Mkoa  wa Geita. Vyerehani hivyo vyenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 87.5 vimetolewa kwa Kata zote za Mkoa wa Geita.  Pamoja na Vyerehani hivyo, Mbunge Vicky Kamata amekabidhi Shilingi Milioni 17.5 kwa  ajili ya kutunisha Saccos za Akina Mama wa kata zote za mkoa wa Geita. Sambamba na hilo Mh. Vicky Kamata ametoa Chupa za Chai  360 kwa akina mama kwa ajili ya kuinua mitaji ya baadhi ya wamama lishe ili kusaidia kuinua vipato vyao. Akikabidhi vyerehani, fedha pamoja na chupa za chai kwa akina Mama hao Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabrieli amempongeza Mh. Vicky Kamata (Mb) kwa upendo aliounyesha kwa kina mama na kwa jamii ya wananchi wa Mkoa wa Geita kwa kuwajali wanawake na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuleta maendeleo. &q

SINGIDA: MBUNGE SIMA AKABIDHI MASHINE YA PHOTOKOPI YA ZAIDI YA MILIONI 3, NA MIFUKO 300 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI KITUO CHA AFYA KISAKI

Image
Na Shams Kunge. Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Musa Sima amekabidhi Mashine ya kutolea Kopi (Photocopy Machine) yenye thamani ya Milioni tatu (3000,000/= ili kuwapunguzia Wazazi na Walimu garama za kwenda kutoa kopi za kulipia, mashine hiyo ameikabidhi kwenye sherehe ya Mahafali ya Kidato cha Nne 2019 Shule ya Sekondari Mufumbu iliyofanyika Tarehe 17.November 2019. Sambamba na hilo Mhe. Sima amekabidhi Mifuko 300 ya Saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kisaki. "Niwaombe wadogo zangu, wanangu na hususani wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mufumbu vidato vyote someni kwa bidii na msome kwelikweli kwani Elimu kwasasa haina Mbadala na tusitanie kwenye hili, lakini pia niwatake Walimu kuhakikisha mnawalea kikamilifu wanafunzi wetu na hilo sio ombi kwani ninyi ni mashahidi Serikali inatoa fedha nyingi za Elimu bila Malipo na kila mwezi shule inapokea fedha za fidia ya ada na Mahitaji mengine mengi,

SINGIDA: BARAZA LA MADIWANI IKUNGI LAZITAKA KAMPUNI ZILIZONUNUA PAMBA KWA WANANCHI KUWALIPA FEDHA ZAO KABLA YA NOVEMBA 30/2019

Image
SINGIDA:  Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi limezitaka Kampuni zilizonunua Pamba kwa wakulima wilayani humo kuwalipa mara moja wakulima fedha wanazo dai kabla ya mwisho wa mwezi novemba 2019 kwani msimu wa kilimo umefika watashindwa kuandaa mashamba yao kama watakua hawajalipwa fedha hizo. Akiongea kwenye Baraza lililofanyika tarehe 13.11.2019 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Diwani wa Kata ya Mtunduru Mhe. Ramadhani Mpaki ameitaka Kampuni ya ununuzi Pamba ya Biosustain kufanya hivo mapema ili kutowakatisha tamaa wakulima kuendelea na kilimo hicho, kwa upande wake Makamu Mwenyeketi wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Issuna Mhe. Missai amewataka wakulima kuandaa mashamba yao mapema ili kuwahi msimu wa mvua unatotarajiwa kuanza hivi karibuni. Nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi amewahakikishia wakulima kulipwa fedha zao kwani atafuatilia kwa ukaribu maagizo ya Baraza. Swala la kulipwa fedha wakulima Lilijiri baada

SINGIDA: MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI MHE. MIRAJI MTATURU ATOA MILIONI 3 KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA ISSUNA - IKUNGI

Image
SINGIDA:  Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu Ametoa Shilingi Milioni tatu ili kuongezea Kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Issuna Wilayani Ikungi. Akiongea kwenye Mkutano na wananchi uliofanyika tarehe 02.11.2019 nje ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Issuna, amesema atahakikisha anapeleka kilio cha wananchi mahali husika ili wananchi waweze kupata huduma zote za afya katika maeneo yao. Aidha Mbunge Mtatutu amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuchagua viongozi waadilifu na watakao mpatia yeye ushirikiano wa kuwawakilisha wananchi na kutoa printer moja kwa ajili ya kuboresha huduma katika Shule ya Msingi Inang'ana Jimboni humo. 

GOOD NEWS: MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI MHE. MTATURU ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA MAPADRI KIBAONI SINGIDA

Image
Na bazil Mjungu: SINGIDA : Mbunge Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ameshiriki uzinduzi wa album ya Pili ya kwaya ya Bikra Maria Mama wa Mungu Parokia ya kibaoni Singida iliyopewa jina la Siri ya Mungu na Kuuza Cd na kufanikisha kupatikana kwa fedha zaidi ya Tsh milioni 4. Uzinduzi: Mtaturu akikabidhi CD alioizindua. Mhe. Mtaturu akimkadhi Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ikungi Ndg. Pius Sankha. Mbali na kiasi hicho cha fedha Mhe. Mtaturu alipata wasaa wa kutembelea jengo linaloendelea kujengwa watakalo ishi Mapadri na kujionea juhudi zilizofikia za ujenzi na kuamua kuchangia mifuko100 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya hiyo ya Mapadri. Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Mtaturu amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa kuwa na amani ili kuenzi amani tuliyo iachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. "Kwa hakika Tunaadhimisha miaka 20 tangu kufariki kwa muasisi wa Taifa letu aliyetuachia tunu ya amani, ni wajibu wetu sasa kuhakikisha tunail

NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA AKABIDHI MASHINE YA PHOTOCOPI SEKONDARI YA MANDEWA SINGIDA

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Musa Sima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Ametoa na kukabidhi Mashine ya kutolea kopi katika shule ya Sekondari Mandewa iliyopo Manispaa ya Singida Mkoni Singida, ikiwa ni katika kuhakikisha shughuli za uendeshaji wa shule hiyo haukwami, Akiongea kwenye Mahafali shuleni hapo Naibu Waziri Sima amesema, imefika wakati kila mtu kuelewa umuhimu wa Elimu na kutambua kua elimu haina mwisho hivyo wazazi, walezi na wadau wa Elimu kutosita kutoa ushirikiano katika kuendelea kufikisha huduma muhimu mashuleni. Akikabidhi Machine hiyo Mhe. Sima amewataka Wadau mbalimbali Nchini kufika maeneo walikosoma au kwenye Shule zenye changamoto na kuona ni jinsi gani kuweza kuzipunguza changamoto hizo na sio kusubiri tu serikali kwani serikali inapata taarifa kwa kuchelewa. Aidha, Mhe. Sima Amewataka wananchi wa Singida hususani ni wa Jimbo la Singida Mjini kushiriki kikamilifu shughuli za maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Mhe

WAZIRI MKUU MHE. KASIM MAJALIWA AFURAHISHWA NA SHUGHULI ZA KIWANDA CHA PAMBA CHA BIOSUSTAIN SINGIDA

Image
Na: Bazil Mjungu. SINGIDA : Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa ametembelea Kiwanda cha kusindika Pamba cha Biosustain kilichopo mjini Singida na kufurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho. Waziri Mkuu amefika na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo na kuonyesha kuridhishwa na Utendaji kazi wa kiwanda hicho. Waziri Mkuu KASIM MAJALIWA amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutumia dawa za asili ikiwemo ndulele na molases ili kuua wadudu waharibifu wa zao la pamba jambo ambalo limeongeza uzalishaji maradufu wa zao hilo. Waziri Mkuu pia amekitaka kiwanda hicho kununua Pamba kwa wakulima kwa bei nzuri ili kuinua kipato cha Mtanzania na kuhimiza  uongozi wa kiwanda cha Biosustain kuzingatia kulipa watumishi wao mishahara mizuri ili kuongeza morari ya kazi.      Akisoma taarifa fupi ya Kampuni hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Biosustain Tanzania Limited Dkt. Riyaz Haider amesema Kampuni ya Biosustain ilianza msimu wa uzalishaji wa Pamba mnamo mwaka 2006/20