GOOD NEWS: MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI MHE. MTATURU ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA MAPADRI KIBAONI SINGIDA
Na bazil Mjungu:
SINGIDA: Mbunge Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ameshiriki uzinduzi wa album ya Pili ya kwaya ya Bikra Maria Mama wa Mungu Parokia ya kibaoni Singida iliyopewa jina la Siri ya Mungu na Kuuza Cd na kufanikisha kupatikana kwa fedha zaidi ya Tsh milioni 4.
Uzinduzi:
Mtaturu akikabidhi CD alioizindua.
Mhe. Mtaturu akimkadhi Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ikungi Ndg. Pius Sankha.
"Kwa hakika Tunaadhimisha miaka 20 tangu kufariki kwa muasisi wa Taifa letu aliyetuachia tunu ya amani, ni wajibu wetu sasa kuhakikisha tunailinda na kuenzi tunu hii, mimi binafsi ninawaomba viongozi wetu wa dini muendelee kutusaidia kuliombea Taifa letu, bila kusahau kumuombea Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli anayefanya kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo watanzania wote bila kujali itikadi zetu.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia ya Kibaoni Padre Patrick Nkoko amemshukuru Mbunge huyo kwa kukubali kujumuika katika tukio hilo na kuahidi kuendelea kuliombea Taifa na kuahidi kua bega kwa bega kuhakikisha waumini wanatoa ushirikiano kushiriki shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
"Tukushukuru kwakweli bila kuficha furaha niliyo NATO wewe Mbunge kukubali mwaliko wetu wa kuja kushirikiana nasi kwenye jambo hili jema la kuendeleza neno la Mungu kwa njia ya uimbaji, umekuwa ni mwepesi kila mahali unapoalikwa hii inaonyesha kuwa wewe ni mtu wa watu na una upendo mkuu sana" alisema padri Nkoko.
Aidha. Mhe. Mtaturu amewashukuru waalikwa na waumini kwa kushiriki vema katika zoezi hilo.
#bazilmjungu.
Comments
Post a Comment