MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI AMSHUKURU MAKAMU WA RAIS KWA KUTOA FEDHA KUKAMILISHA JENGO LA ZAHANATI ULYAMPITI


Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu amemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  kwa kutoa Fedha kiasi cha shilingi milioni 154 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ulyampiti Wilayani Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki.

Mbunge huyo amesema Makamu wa Rais alipofanya ziara ya kikazi hapo mwishoni mwa Mwaka 2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi yeye akiwa Mkuu wa Wilaya hiyo aliona ni jinsi gani wananchi wa Kijiji cha Ulyampiti wakitaabika kupata huduma za afya na kuamua Kumuomba mbele ya wananchi asaidie fedha za umaliziaji ujenzi wa Jengo la Zahanati hiyo ili kuweka karibu huduma ya Mama wajawazito, watoto wadogo na Wazee kuliko kufata huduma hiyo Ikungi, Itigi na Mkoani Singida.

Akiongea na wananchi hao wa Kijiji cha Ulyampiti Mhe. Mtaturu amemshukuru Makamu wa Raisw Mhe. Samia Suluhu Hassani Pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa Kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Ulyampiti kiasi cha Milioni 154 kwa ajili ya umaliziaji wa Zahanati ya Kijiji hicho. 

Aidha Mtaturu amewataka wananchi wa Kijiji hicho kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli kama ambavyo amefanya yeye kuleta fedha za zahanati hiyo na imeanza kutoa huduma kwa wananchi na kuwafanya wananchi wa Kijiji hicho kutosafiri kwenda mbali kufuata huduma za matibabu.

Mhe. Mtaturu amewataka wananchi hao kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi watakao baini na kufuatilia kwa ukaribu shughuli za maendeleo na sio viongozi wa kujaza nafasi.


Na Bazil Mjungu:
#bazotv


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida