WAZIRI MKUU MHE. KASIM MAJALIWA AFURAHISHWA NA SHUGHULI ZA KIWANDA CHA PAMBA CHA BIOSUSTAIN SINGIDA

Na: Bazil Mjungu.
SINGIDA: Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa ametembelea Kiwanda cha kusindika Pamba cha Biosustain kilichopo mjini Singida na kufurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho.

Waziri Mkuu amefika na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo na kuonyesha kuridhishwa na Utendaji kazi wa kiwanda hicho.

Waziri Mkuu KASIM MAJALIWA amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutumia dawa za asili ikiwemo ndulele na molases ili kuua wadudu waharibifu wa zao la pamba jambo
ambalo limeongeza uzalishaji maradufu wa zao hilo.

Waziri Mkuu pia amekitaka kiwanda hicho kununua Pamba kwa wakulima kwa bei nzuri ili kuinua kipato cha Mtanzania na kuhimiza 
uongozi wa kiwanda cha Biosustain kuzingatia kulipa watumishi wao mishahara mizuri ili kuongeza morari ya kazi.  
  
Akisoma taarifa fupi ya Kampuni hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Biosustain Tanzania Limited Dkt. Riyaz Haider amesema Kampuni ya Biosustain ilianza msimu wa uzalishaji wa Pamba mnamo mwaka 2006/2007 kwa kuhamasisha wananchi kulima Pamba baada ya zao hill kufa mwaka 1998, ambapo mwaka 2006/2007 Kampuni ilianza kuhamasisha kilimo hicho katika Kijiji cha Iglansoni Wilayani Ikungi na kuzalisha tani 165 tu.

Dkt. Riyaz Haider aliongeza kwa kusema "Mhe. Kasim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania, mwaka huu tunatazamia kuvuna Pamba zaidi tani 6,000. Ikiwa yote imenunuliwa kwa asilimia 90, na iliyobakia tunategemea kuimaliza katikati ya Mwezi huu wa 10.2019 na uzalishaji kwa Nchi nzima tunategemea kuvunja rekodi kwa kuvuna takribani tani 400,000".

Aidha Dkt. 
Riyaz Haider ameipongeza Serikali ya Awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuipeleka Nchi ya Tanzania katika Uchumi na Viwanda, na kumshukuru Waziri Mkuu kwa jitihada kubwa za kusukuma uzalishaji wa mazao ya kimkakati.

Waziri Mkuu yupo Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku NNE, ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

@bazotvnews.

#WhatsApp#youtube. Bazo TV online

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida