NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA AKABIDHI MASHINE YA PHOTOCOPI SEKONDARI YA MANDEWA SINGIDA


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Musa Sima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Ametoa na kukabidhi Mashine ya kutolea kopi katika shule ya Sekondari Mandewa iliyopo Manispaa ya Singida Mkoni Singida, ikiwa ni katika kuhakikisha shughuli za uendeshaji wa shule hiyo haukwami,

Akiongea kwenye Mahafali shuleni hapo Naibu Waziri Sima amesema, imefika wakati kila mtu kuelewa umuhimu wa Elimu na kutambua kua elimu haina mwisho hivyo wazazi, walezi na wadau wa Elimu kutosita kutoa ushirikiano katika kuendelea kufikisha huduma muhimu mashuleni.

Akikabidhi Machine hiyo Mhe. Sima amewataka Wadau mbalimbali Nchini kufika maeneo walikosoma au kwenye Shule zenye changamoto na kuona ni jinsi gani kuweza kuzipunguza changamoto hizo na sio kusubiri tu serikali kwani serikali inapata taarifa kwa kuchelewa.

Aidha, Mhe. Sima Amewataka wananchi wa Singida hususani ni wa Jimbo la Singida Mjini kushiriki kikamilifu shughuli za maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli,

"Niwaombe tu ndugu zangu wana manispaa ya Singida tuwe na umoja wa na ushirikiano kwa kila pande ili tuweze kuijenga Singida yetu, naamini tukiungana tutafanya vizuri sana, na kwakua Mimi ni Naibu Waziri basi kero mlizo nieleza nitahakikisha nazifikisha mahali husika" alisema Mh. Sima.

#bazotvnews.

Naibu Waziri.

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida