MVUA YASABABISHA UHARIBIFU WA MASHAMBA YA KAYA 93 RORYA MARA
ROYRA MARA:
Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyo nyeesha Desemba 12/2019 katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilayani Rorya Mkoani Mara imesababisha maporomoko makubwa ya mawe na mmomonyoko mkubwa wa ardhi hali iliyopelekea kuharibika kwa mashamba ya Kaya zaidi ya 93.
Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo (CCM) alitembelea eneo hilo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Charles Ochele na viongozi wengine wa Serikali za Vijiji na Kata kufika katika eneo la tukio na ujionea uharibifu mkubwa Mashamba kusombwa na Maji yenye Mawe Makubwa yaliyosababisha kutokea kwa mto na bonde kubwa huku za zaidi ekari 20 za mazao ya wananchi kusombwa na maji na kuharibiwa na mamia ya mawe yaliyoporomoka kutoka zaidi ya km 2 kutoka eneo la Mashamba n Mlima uliko.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Tatwe Mhe. Lameck Airo ametoa pole kwa wananchi na kuonyesha kusikitishwa na tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi na kuwashitua wananchi zaidi 93 kuharibiwa mazao katika kwa uharibifu ikiwemo baadhi ya Nyumba kupata nyufa kutokana na Maporomoko hayo.
"Tukio hili limetokea majira ya saa 11:00 jioni Desemba 12 na limeacha janga na hali ya wasiwasi baada ya kuporomoka kwa mawe makubwa na uharibifu wa ardhi amapo eneo hili limekuwa na mto mkubwa ambao unatiririsha maji hadi mto Chirya haya ni maajabu lakini tushukuru Mungu hayakulenga makazi ya wananchi tungeshuhudia mamia kupoteza maisha," alisema Mhe. Airo.




" Mvua hii iliwahi kutokea mwaka 1996 lakini haikuwa na madhara kama hii leo tumeshuhudia maafa na mazao kusombwa na mawe na mchanga na tumeshuhudia nyumba mbili zikianguka na ng'ommbe wawili wakisombwa ni jambo ambalo limetuweka katika wasiwasi mkubwa na kuhofia maisha yetu hivyo tunaomba wataalam waje kufanya utafiti kutambua kilichotokea ama kilichosababisha" Alisema Rosemary Joseph.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Tatwe, Julius Ochwachi aliwashukuru Mbunge Airo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ochele kwa kufika na kutembelea eneo la tukio huku wakiguswa na kutoa msaada kwa waathirika kumi waliopoteza nyumba na mifugo yao huku wananchi wengine 83 wakiwa wameshuhudiwa wakipoteza mazao ya mahindi, mtama, ulezi, mihogo, viazi vitamu, mpunga na maharage katika maeneo mashamba yao zaidi ya ekari 20 huku mapolomoko hayo yakiwa na urefu wa km 2 kutoka eneo la tukio hadi mto Chirya.
:Picha Na Peter Fabian
#Bazotv
Comments
Post a Comment