Tamko la vyama vya siasa 10 limetolewa Dodoma kupiga matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na Chadema na washirika wao kupinga Mabadiliko ya Vyama vya Siasa pamoja na Juhudi anazofanya Mhe Rais Dr John Pombe Magufuli. Leo Jijini Dodoma limetolewa tamko linalopinga siasa chafu ambazo zimekuwa zikifanywa na Chadema pamoja na washirika wao kupinga juhudi na Kazi nzuri anazozifanya Mh Rais. Aidha tamko hilo linapinga upotoshaji unaofanywa na baadhi ya vyama siasa dhidi ya Mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa. Tamko hilo limetolewa na Vyama kumi na moja ambavyo ni CUF,TLP,ADC,DP,NRA,AAFP,UMD,SAU UDP,na DEMOKRASIA MAKINI. Vyama hivyo vimeeleza kuwa vinasikitishwa na namna Mataifa ya Kigeni yanavyotoa fedha kudhamini mambo yanayolenga kuchafua taswira ya Taifa kupitia baadhi ya vyama vya Upinzani kama CUF SEIF na CHADEMA lengo likiwa kuichafua serikali ya Mhe Rais Magufuli anayepambana kuleta maendeleo. Imeelezwa kuwa wanayo taarifa kuwa mikataba ya madini iliyobadilishwa na Serikali na kuan