IKUNGI. SERIKALI KUCHIMBA VISIMA VYA MAJI KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI

Ziara DC Ikungi Day 3:

Tumeendelea kuwafikia wananchi kukagua miradi na kuhamasisha maendeleo Vijiji vya Damankia na Samaka.

Maagizo/Utatuzi changamoto na Pongezi; 

1.Wananchi wamelalamikia Uongozi wa kijiji cha Damankia kutowasomea mapato na matumizi na kudhoofisha maendeleo ya kijiji ikiwemo maendeleo ya shule,DC Mtaturu amemwagiza DED aitishe mkutano wa wananchi wote kujadili changamoto hiyo kufikia tarehe 30 Octoba.

2.Miradi ya kijiji cha Samaka;Ofisi ya Serikali kijiji na Ujenzi wa Matundu 12 ya Choo Shule ya msingi wananchi wamefyatua matofali 9000.

DC amewaunga mkono wananchi matofali 500 na saruji mifuko 20 kusaidia kumalizia ujenzi wa Ofisi ya Kijiji,Mabati 30 kupaua matundu 12 ya Vyoo,magoli ya chuma kwenye uwanja wa mpira na mipira miwili kwa ajili ya wanafunzi.

3.Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto DC Mtaturu ameagiza wakati mpango wa  ujenzi wa zahanati DED alete wauguzi mara moja kwa mwezi Samaka kliniki kwa ajili ya akina mama na watoto kuwapunguzia umbali kwenda Dung'unyi zaidi ya km 5.

4.Kila kaya kupanda miti 10 kila mwaka kwa ajili ya hifadhi ya mazingira na kutakata miti hovyo.

5.Pongezi kwa Shule ya msingi Samaka kutekeleza mpango wa lishe shuleni.

6.Serkali mwaka huu kuchimba visima virefu vya maji Samaka,Damankia,

Munkinya na Kipumbuiko ikiwa ni kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani.

7.Wananchi wameishukuru serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais mhe. Dkt. John Pombe kuwaletea mradi wa REA utakaogusa vijiji vya Kipumbuiko,Damankia na Samaka vilivyopo kata ya Dung'unyi.

8.Wananchi wamepongeza Mkuu wa wilaya kwa juhudi za kusimamia maendeleo katika wilaya na hakika wameahidi maagizo na ushauri wake watayazingatia ili kujiletea maendeleo.

9.DC Mtaturu amewachangia vikundi vya Vicoba Uaminifu na Upendo laki 2 kila kimoja kuongeza mtaji ili waendelee kukopeshana.

Ziara inaendelea kuwafikia wananchi kusikiliza kero na changamoto zao.

"IkungiYetuSote#TuijengePamoja#

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida