TATIZO LA MAFUTA IKUNGI KUISHA

Leo tarehe 30 Octoba,2018  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amekagua ujenzi wa kituo cha mafuta kinachojengwa Makao Makuu ya Wilaya.

Huduma ya mafuta ni changamoto kubwa Kwenye uendeshaji wa shughuli za kila siku za Serikali na watu binafsi ikiwemo Huduma za usafirishaji abiria, Inatulazimu kwenda km 40 hadi Singida mjini kupata Huduma ya mafuta.


Dc mtaturu amemshukuru sana ndugu Farid Bazaar kukubali ombi la wilaya la  kuwekeza kwa kujenga kituo cha mafuta na matarajio kianze kutoa Huduma mwishoni mwa Novemba 2018.


Aidha DC Mtaturu ameongeza kwa kusema, Wananchi wanapaswa kuelewa maana ya uwekezaji ili kuwapa ushirikiano na kuleta huduma kwa wananchi,

"Kwa wilaya yetu Mara nyingi wanapotokea wawekezaji wamekua hawapewi ushirikiano na kusababisha mitafaruku kati ya wamiliki  wa maeneo na mwekezaji na kuwafanya wawekezaji kuogopa kuja kuwekeza katika wilaya yetu kitu ambacho kimetufanya kuwaelekeza wananchi kuelewa maana ya neno mwekezaji"

Hakika uongozi bora ni kwa vitendo.

"IkungiTunayoitamani#ImekaribiaTushikamanePamoja"

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida