DC Mtaturu. Chuo cha VETA kujengwa Ikungi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Amewataka wazazi kuwahimiza wanafunzi kuhudhuria vizuri katika masomo ili kuleta ufaulu mzuri katika wilaya ya Ikungi na Mkoa kwa ujumla.
Akihutubia kwenye mahafali ya kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Siuyu, Mtaturu amewaomba wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuhakikisha kwa pamoja wanatokomeza utoro usio wa lazima kwa wanafunzi,
Aidha, DC Mtaturu akasema " kutokana na ufaulu unaonyesha 20% tu ya wanafunzi ndio hufaulu kujiunga na vyuo ama kidato cha tano, na kubakiza 80% ya waliofeli masomo na kubaki nyumbani wakiwa hawana chochote cha Serikali ya wilaya ya Ikungi imeamua kujenga chuo cha Veta ili wanao baki hawa 80% wajiunge na chuo hicho na itafanya wapate fani mbalimbali ili kujikimu katika maisha yao"
Mwisho akawataka walimu kujituma zaidi ili kuongeza ufaulu wa shule hiyo.
Comments
Post a Comment