Posts

Showing posts from 2018

IKUNGI: WAZEE WA IKUNGI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA Mhe. MIRAJI J. MTATURU KWA KUSIMAMIA MAENDELEO KWA UZALENDO WA KIPEKEE

Image
Wazee Wa Ikungi wampongeza Mkuu wa Wilaya Mhe Miraji J.Mtaturu kwa kusimamia Maendeleo kwa wananchi kwa miaka miwili Ikungi yasonga mbele kimaendeleo na Amani na Utulivu yatawala.  Wamuombea makubwa zaidi na waahidi kumuunga mkono ili atimize malengo ya Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

IKUNGI: DC MTATURU AAGIZA KUUNDWA KAMATI YA KURATIBU MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI IKUNGI

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Ameagiza kuanzishwa kwa Kamati ya Kuratibu na kusaidia Vyama vya watu wenye ulemavu Wilayani Ikungi. Akiongea katika Mkutano huo Bi. Ummy Nderiananga Mwenyekiti wa SHIVYAWATA  Taifa, amesema umefika muda sasa wa kujua umuhimu wa kuwapa kipaumbele na kuwajumuisha ipasavyo  watu wenye Ulemavu  wa aina zote ili kutambulika na wao kujitambua kuwa taifa linawategemea.Ametoa Mfano wa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli alivyowajumuisha watu wenye ulemavu Kwa kuwateua kushika nafasi mbalimbali za maamuzi Serikalini.Huo ni Mfano chanya unaopaswa kuigwa na Viongozi wengine wa serikali katika maeneo yao mbalimbali  ya kazi. Akisoma taarifa fupi kutoka Idara ya Elimu, Elimu Maalum, Afisa Elimu, Elimu Maalum Ndg. Peter Ngatunga, taarifa iliyo onyesha Chama Cha watu wenye Ulemavu kutopata ushirikiano kikamilifu kutokana na kutokuwepo wafuatiliaji wa karibu (Kamati) inayoweza kutambua kwa urahisi mahitaji ya Walemavu Na kumfanya Mkuu wa Wilay

DODOMA: VYAMA KUMI VYA UPINZANI VYATOA TAMKO KALI KUUNGA MKONO MABADILIKO SHERIA YA VYAMA VYA SIASA, VYASEMA RAIS NI JEMBE. AUNGWE MKONO.

Tamko la vyama vya siasa 10 limetolewa Dodoma kupiga matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na Chadema na washirika wao kupinga Mabadiliko ya Vyama vya Siasa pamoja na Juhudi anazofanya Mhe Rais Dr John Pombe Magufuli. Leo Jijini Dodoma limetolewa tamko linalopinga siasa chafu ambazo zimekuwa zikifanywa na Chadema pamoja na washirika wao kupinga juhudi na Kazi nzuri anazozifanya Mh Rais. Aidha tamko hilo linapinga upotoshaji unaofanywa  na baadhi ya vyama siasa dhidi ya Mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa. Tamko hilo limetolewa na Vyama kumi na moja ambavyo ni CUF,TLP,ADC,DP,NRA,AAFP,UMD,SAU UDP,na DEMOKRASIA MAKINI. Vyama hivyo vimeeleza kuwa vinasikitishwa na namna Mataifa ya Kigeni yanavyotoa fedha kudhamini mambo yanayolenga kuchafua taswira ya Taifa kupitia baadhi ya vyama vya Upinzani kama CUF SEIF na CHADEMA lengo likiwa kuichafua serikali ya Mhe Rais Magufuli anayepambana kuleta maendeleo. Imeelezwa kuwa wanayo taarifa kuwa mikataba ya madini iliyobadilishwa na Serikali na kuan

IKUNGI: KIKUNDI CHA VUMILIA VIKOBA MAKIUNGU WASHEREHEKEA KUMALIZA MZUNGUKO WA AWAMU YA TATU (3)

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Ameshiriki Sherehe ya Kumaliza mzunguko wa awamu ya  Tatu (3) wa Kikundi cha Vumilia VIKOBA Makiungu mzunguko ulioonyesha kuwa na faida kubwa kuliko mizunguko miwili (2) iliyopita. DC MTATURU amekipongeza kikundi hicho kwakua na Upendo mkubwa, Umoja na kuwa na Uongozi uliotukuka ambao umekifanya Kikundi hicho kuwa na uchumi mzuri uliopelekea kujikomboa na kujitosheleza katika kusaidia familia zao, Pia Dc Mtaturu, a mewataka kuanzisha Mradi kiwanda Kidogo ili kuweza kuongeza kipato kwa wanakikundi na Kuongeza huduma kwa jamii jambo ambalo litawafanya wasiopenda kujiunga na vikundi wahamasike zaidi. Aidha, Dc Mataturu amewataka wanakikundi hao kujiunga na Bima za afya ili kuepuka garama zinazo jitokeza pale mtu anapo ugua gafla, kadhalika Dc Mtaturu amewaomba  wasiwe na ubinafsi ili vikundi vingine vidogovidogo viweze kuja kukopa katika kikundi chao na Uchumi wao utakua umekua na kuimarika zaidi. Mhe. Miraji Mtaturu Mkuu wa

TANZANIA: MBOWE KUENDELEA KUTESEKA GEREZANI NI UDHAIFU KWA UPINZANI

Na Kibona Dickson. (Mchambuzi huru). Mwenyekiti wa chadema taifa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni yuko gerezani kwa siku kadhaa.Anaweza kuendelea kubakia huko mpaka mwakani kwa sababu tumesikia korti zinaenda likizo mpaka mwakani.Kuna walakini kama rufaa ya upinzani itasikilizwa na uamuzi kufanyika mapema. Kwa kumtia Mbowe gerezani,watawala wana akili za kuchungulia ili kuona aina ya upinzani uliopo nchini  kwa sasa ili baadaye waweze kufanya Mambo yao bila kusikiliza kelele za chura. Tukio la   Mbowe kuwekwa rumande ni litmus paper ya watawala.Wamesoma mchezo wa upinzani.Siku zimeenda bila joto la  kisiasa kupanda nchini.Mbowe kiongozi wa chama kikubwa anaendelea kuteseka gerezani.Wafuasi wa chama kikubwa hawana la  kufanya zaidi ya kuandika mtandaoni.Watawala wameshajua litmus paper yao inasomeka "upinzani ni dhaifu kwa sababu wafuasi wa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani hawana la  kufanya." Yule mgombea urais mwenye mamilioni ya wafuasi kashapewa kejeli "ne

SINGIDA: SERIKALI YATOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) 2016-2018

Image
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu. Akisoma taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Singida Dr. Rehema Chimbi. Kaimu huyo wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Akisoma taarifa hiyo  kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Singida Dr. Rehema Chimbi, Ameelezea kwa undani Vitu vilivyo tekelezwa na Serikali ya Mkoa katika kutimiza wajibu wake kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Singida. Akiw asilisha taarifa kwa niaba ya mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu   mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Singida.  amesema kwa kipindi cha miaka miwili mwaka 2016-2018 Ilani imetekelezwa vizuri kwenye sekta za Elimu, Afya, Maji, Miundombinu na Ulinzi na Usalama. Aidha. Amempongeza Rais mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa maelekezo yake na kuleta fedha za miradi ya maendeleo iliyosababisha kutekeleza miradi yote ikiwemo vituo vya afya 10 vinavyoendelea kujengwa kwenye halmashauri zote za mkoa

IKUNGI: KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA WILAYA (DCC) CHA AZIMIA KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Image
Kamati ya ushauri ya Wilaya DCC Ikungi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, ambaye ni Mkuu wa wilaya Ikungi , na Katibu wa kikao Ndg Justice Lawrence Kijazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri   wilaya ya Ikungi. Kamati hii imekaa   kwa mara ya kwanza tangu Halmashauri hiyo kuanzishwa Mwaka 2013 ambapo imejadili mambo mbalimbali ya maendeleo. Katika kikao hicho Mada zilizo pamba moto ndani ya ukumbi zilikua kama  Maswala ya kilimo bora chenye kuzingatia maelekezo ya wataalamu ili kuleta tija. Usimamizi wa Utawala bora. Kujitambua kama Mtumishi wa serikali na mwananchi kutambua wajibu wake. Kusimamia Sheria na kutekeleza maagizo ya Serikali. Uhaba wa Madawati katika shule zote za Msingi na Sekondari. Vifo vya Mama na Mtoto,   Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya pamoja na Utokomezaji wa Mimba na Ndoa za utotoni. Baada mjadala kuendelea kulijitokeza kauli zilizo onyesha dhahiri kua kuna viongozi wanaozuia wananchi kushiriki katika kazi za mae

IKUNGI: KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA YATINGA IKUNGI KUKAGUA MIRADI YENYE THAMANI YA 4.2 BILIONI.

Image
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida, Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Mhe. Juma Kilimba Imefika Wilayani Ikungi Kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Tsh 4.2 Bilioni ikiwemo Ofisi na Nyumba ya kuishi Mkuu wa Wilaya, Majengo ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Zahanati ya Kijiji cha Mang'onyi,  Nyumba ya Walimu Lighwa Sekondari, Kiwanda Kidogo cha Chaki cha Vijana wa Mwisi na Kutembelea kituo cha Polisi cha Mang'onyi ikiwa ni kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi unasimamiwa ipasavyo. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida. Mhe. Juma Kilimba akiipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo ongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli    kwa kazi nzuri aliyojionea mwenyewe katika Wilaya ya Ikungi. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. MIRAJI Jumanne Mtaturu akiipongeza Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi mkoa kwa utayari wao wa kukijenga Chama na kuanza ziara ya kukagua miradi. DC MTATURU Akitoa taarifa fupi