TAARIFA MUHIMU KWA WANANCHI WA JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Napenda kutoa taarifa rasmi kwa wananchi wa *Jimbo la Singida Mashariki* kuhusu Bajeti ya *Mwaka 2021/22* kwenye Jimbo letu *,Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan* imetutengea *Tsh Bilion 1.5* kwa ajili ya kufungua Barabara mpya ambazo hazijawahi kufunguliwa kabisa,Ujenzi wa madaraja na kuziimarisha zilizopo ili kurahisisha mawasiliano ndani ya Jimbo pamoja na shughuli za kiuchumi.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa *Ilani yetu ya CCM 2020- 2025* ambayo pamoja na mambo mengine imeahidi kuendeleza shughuli za ujenzi wa miundombinu mbalimbali Ili kuifanya sekta hiyo ifikie malengo yake ya kuwezesha wananchi kuendelea na uzalishaji kwa ajili ya kuongeza kipato chao.
Hivyo Basi, Baada ya kushauriana na Meneja wa TARURA tumekubaliana Barabara zifuatazo zitengenezwe;
1.Misughaa-Msule-Sambaru km 27.90 Tsh Milioni 600.
2.Mungaa-Ntuntu-Mang'onyi km 15 Tsh milion 330.
3.Siuyu-Nali-Makotea km 7.26 Tsh Milion 280.
4.Utaho-Makiungu Km 12.71 Tsh Million 290.
Ikumbukwe hii ni nje ya zile fedha za Bajeti za kawaida ambazo pesa zimetolewa na barabara zingine zitaendelea kutengenezwa kama ifuatavyo;
1.Mungaa-Ntuntu-Mang'onyi km 5 Tsh milion 152.
2.Mkiwa-Choda Km 5 Tsh 41.75
3.Nkuhi-Manjaru km 5 Tsh milion 77.
4.Matare-Kinyamwandyo Drift 1 Tsh milion 35.
5.Issuna-Ng'ongosoro-Ilolo km 10 Tsh milion 46.52
6.Mungaa-Dung'unyi-Ikungi km 12 Tsh 78.5
Hakika tunaishukuru sana Serikali kwa dhamira yake ya kutengeneza miundombinu muhimu ya barabara itakayochochea shughuli za kiuchumi na kurahisisha utoaji huduma vijijini hii ndio maana halisi ya kutoa huduma kwa Wananchi. 👏🙏
Nawasilisha
Ndimi Mtumishi Wenu;
*
*Miraji Jumanne Mtaturu* *(MB)*
*Singida Mashariki*
*17 July, 2021**
#MaendeleoYetu#KipaumbeleChetu#SingidaMashariki#KaziIendelee#
Comments
Post a Comment