KINGU NA WANANCHI WA JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI, MIUNDOMBINU YA BARABARA JIMBONI

Na Elibariki Kingu (Mb)
Napenda kuwataarifu Wananchi wote wa Jimbo la Singida Magharibi; kuwa. Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeshaelekeza TARURA Mikoa na Wilaya kuainisha Barabara zitakazo jengwa kwa nyongeza ya bajeti ya Tshs Bilion moja tuliyopewa.

Barabara zetu za Jimbo la Singida Magharibi zitakazojengwa kwa kiwango Cha MORAMU ni kama ifuatavyo:-

1. Barabara ya Isuna - Ngo’ngosoro hadi Ilolo KM 8. Milion 250: jina la Barabara haimaanishi tunajenga upande wa isuna hadi Ng'ongosoro hapana, bali ni upande wa Singida Magharibi unaopakana na Ngo’ngosoro.

Lengo ni watu wetu wafike Ikungi bila kuja mpaka puma na barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa watu wetu:

2. Mtamaa -Minyughe - Mtavira urefu KM 4 na daraja lililokatika huko Makilawa milioni (330M:) haimaanishi tutajenga mtamaaa maana ni ya mjini bali ni jina la barabara, pesa zitatumika kujenga upande wa Kata ya Minyughe na Makilawa, Barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa Kata hizi mbili kwa usafirishaji wa mazao ya kilimo na biashara na hata Wananchi kufika Singida kufata nahitaji yao.

3. Ighombwe - Makhonda - Mwaru KM 13. Milioni (330M) watu wetu wa Makhonda wameteseka sana sana wakati wa mvua hapa tutainua tuta na kujenga daraja hadi Makhonda kwa awamu ya kwanza

4. Sepuka - Italala KM 2.1 Milioni 90 Wakazi wa Italala wameteseka kwa miaka wakati wa mvua ili watoke makao makuu ya tarafa lazima wapite iporyo na Msungua kufika italala zaidi ya KM 13 wakati ni umbali wa KM 2 tuu.

Aidha barabara zingine ambazo zitajengwa kwa bajeti halisi ya awali ni:-

Puma - Wibia
Puma - Igelansoni
Minyughe - Mtavira

Mtavira - Mteva hadi Nduru

Wakandarasi wako Maeneo ya kazi na kazi hii inafanyika kwa kasi sana kwa utekelezaji utakao leta tija kwa walengwa.

Niwatake Wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi, Kuwapokea Wakandarasi wote watakao fika Katika maeneo yao na kuwapa ushirikiano.

Elibariki Immanuel Kingu (Mb)
Jimbo la Singida Magharibi

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida