NAIBU WAZIRI TAMISEMI MWITA WAITARA AWASHUKIA WENYEVITI WASIO NA SIFA YA UONGOZI
Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mwita Waitara (Mb), amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliomaliza muda wao ambao walikuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kashifa za migogoro hasa ya ardhi, wasijihangaishe kujuchukua fomu za kugombea nafasi hizo kwani muda waliokua madarakani hawakuweza kuwatumikia Wananchi ipasavyo.
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Waitara haliyasema hayo katika ziara yake ya kikazi katika Jimbo la Ukonga alipoenda kukagua miradi ya Maendeleo sambamba na kusikiliza kero za wananchi.
"Nafasi yenu ya Wenyeviti wa Mtaa ni ya kujitolea mlichaguliwa na wananchi ili muwatumikie muda wenu umekwisha wale Wenyeviti waliosababisha kesi za migogoro ya kuuza ardhi kiholewa na kutumia madaraka vibaya katika serikali ya amamu ya tano hawana sifa ya kuwa kiongozi majina yatakatwa"alisema Waitara..
Waitara aliwataka Viongozi wa chama wahakikishe wanapitisha majina ya watu wanaokubalika na jamii ili wapigiwe kura kwa ajili ya kuja kuongoza wananchi na kushirikiana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ili kuendeleza adhma ya kuijenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.
Aidha Mhe. Waitara aliwataka wananchi wa Jimbo la Ukonga na watanzania kwa ujumla kushiriki uchaguzi huo na kuchagua kiongozi mwenye sifa atakaye weza kuongoza wananchi na kusimamia miradi ya maendelea na kuchukia rushwa kwani ni adui wa haki.
Akizungumzia kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa alisema uchaguzi wa mwaka huu 2019 wagombea Wajumbe sita kati ya wajumbe sita wanawake wawili na Wanaume wanne .
"Katika Ofisi ya Serikali ya Mitaa kuna mambo mengi ya kijamii serikaĺi imeliona ili tumeweka wajumbe wawili ambao watachaguliwa na Wananchi kwa ajili ya kushuruisha migogoro yenu , wagombea watarajiwa nakala hizi zipo kwa Maofisa Watendaji wa kata na Wilayani kwa wakuu wa Wilaya zenu"alisema
Wakati huo huo Waitara alisema Serikali imemaliza mgogoro wa Mpaka wa Magore A kata ya Kivule Manispaa ya Ilala na Temeke hivyo wananchi wa Magore A kuanzia sasa wanahesabika ni wananchi wa Wilaya ya Ilala sakata la mpaka limekwisha.
Katika ziara hiyo Mhe. Waitara amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala kumtafuta Mtendaji wa Magore A ili wananchi wa mtaa huo waweze kushiriki uchaguzi wa mtaa mwaka huu 2019 waweze kupata haki za msingi na huduma za jamiï.
Alisema kama Mbunge wa jimbo la Ukonga na Naibu Waziri wa TAMISEMI mara baada kupata serikali yao Magore A watajengewa zahanati, soko, shule ya msingi, kuwaletea mradi wa maji na umeme wa REA ila wachague Wenyeviti wenye chachu ya maendeleo atakayeweza kuwatumikia Wananchi.
#bazotvnews
Na: Bazil mjungu
Comments
Post a Comment