KISHINDO CHA MTATURU JIMBONI CHAZOA WAPINZANI 13





Jumla ya viongozi na wanachama 13 wa vyama vya upinzani kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kutoka Cha Cha Wananchi (CUF) wamehama vyama vyao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kile walichodai kukubaliana na kasi ya Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuleta maendeleo.

Miongoni mwa wanachama hao Katibu wa CUF Wilaya ya Ikungi Selemani Ntandu aliyekuwa katibu wa kuratibu shughuli za Lissu tangu 2007, mwenyekiti wa CHADEMA katika kijiji cha Ighuka Venance Elias na Katibu wa Chama hicho kata ya Ikungi Zakaria Kadagaa na Ezron Obed Kidumu -CHADEMA  Ikungi.

Akikabidhi kadi kwa wanachama hao wapya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi Mhe. Mika Likapakapa amewataka wanachama hao kuwa waaminifu na watiifu kulingana na kiapo cha ahadi ya mwanachama na kutorudi nyuma katika kuhakikisha wanashiriki vyema kuendelea kukiimarisha chama .



Akizungumza mmoja wa wanachama waliohamia CCM Selemani Ntandu amesema huo ni mwanzo tu lakini shughuli kama hiyo itaendelea.

Mimi ndio nilikuwa katibu wa kuratibu shughuli zote za Lissu tangu Julai mosi 2007 mpaka anapata ubunge kesi inaenda mahakamani nilisimama saa tano kumtetea nikiwa kama shahidi wake,sasa naomba nimtumie salamu huko huko kuwa akitoka Ubelgiji arudi CCM,”alisema  Seleman Ntandu".

#bazotvnews.

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida