MTATURU KUFADHILI WANAFUNZI 200 UNIFORM KILA MWAKA JIMBONI KWAKE
Na Bazil Mjungu.
IKUNGI: Wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi katika mkoa wa Singida wamejitokeza kwa wingi kumpokea Mbunge wao Mhe. Miraji Mtaturu aliyewasili akitokea Bungeni Jijini Dodoma baada ya kumaliza vikao vya Bunge.
Mhe. Mtaturu amelakiwa na Wananchi wa Jimboni humo na kufanya mikutano kadhaa kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake.
Mtaturu aliapishwa septemba 3 2019 Bungeni Dodoma baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Tundu Lissu (CHADEMA) kupoteza ubunge bada ya kukosa sifa kwa kutohudhuria vikao bila ya taarifa na kutojaza fomu za tamko la mali na madeni Bungeni.
Akizungumza katika Mikutano aliyoifanya katika Vijiji vya Mkiwa, Issuna na Ikungi Mtaturu akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (MB) ameahidi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki wanapata maendeleo.
Aidha katika mikutano hiyo ameweka bayana vipaumbele vyake atakavyovitekeleza katika kipindi cha Ubunge wake ambavyo ni Elimu na Kudumisha Asili ambapo atahamasisha jamii kuunga mkono elimu bila malipo pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia na kuwa na Jamii iliyoelimika ndio yenye uwezo wa kujiletea maendeleo,
"Kipindi linipokua Mkuu wa Wilaya hapa nilifanya kazi hiyo, Sasa nitaendelea kuhamasisha jamii yetu zaidi na nitaunga mkono elimu bila malipo kwa kukabiliana na upungufu ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, walimu na ujenzi wa mabweni ili kuokoa watoto wakike kutopata Mimba wakiwa shuleni"
“Katika utumishi wangu ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwangu ni kazi tu, na Serikali inayotekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM inawapenda na kuwajali ninyi wananchi, nitahakikisha tunashirikiana pamoja ili kusukuma mbele gurudumu letu la maendeleo, na katika hili nimekuja na kauli mbiu isemayo, Maneno kidogo, kazi zaidi, hapa kazi tu.
Mhe. Mtaturu aliongeza kwa kusema: “Katika sekta ya elimu nitahakikisha pia kila mwaka nasaidia wanafunzi 200 ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwanunulia sare za shule, ambapo wanafunzi 100 wa shule za msingi na 100 wa Shule za sekondari, nitaomba watendaji wetu wanisaidie katika kuwatambua, nafanya hivi ili kumuunga mkono Rais wetu Dkt John Magufuli” :"alisema Mtaturu"
Aidha, nitawalipia ada wanafuzi 10 waliofaulu kujiunga na kidato cha tano katika shule zetu za Serikali, watano wa kike na watano wakiume, “hili nilishaanza nikiwa Mkuu wa wilaya kuna mtoto alipata daraja la pili kachaguliwa kuendelea na masomo wazazi wake hawana uwezo, niliamu kumsaidia kumlipia hela na mahitaji yake yote karibu laki 7 sasa hivi yupo shuleni” alisema Mtaturu..
Vipaumbele vingine alivyotaja ni kwenye sekta ya maji, afya, kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuhamasisha kilimo cha kisasa badala ya kile cha mazoea na kuanzisha mradi wa kukopesha wananchi Ng’ombe wa maziwa utakaojulikana kama Kopa ng’ombe lipa ng’ombe ambao watasambazwa kwenye tarafa mbili za Jumbo la Singida Mashariki.
Mtaturu Ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. Jojn Magufuli kwa kuwapelekea sh bilioni mbili za ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA) kama alivyoomba akiwa Mkuu wa wilaya ya Ikungi na Kuitengea Wilaya ya Ikungi fedha kwa ajili ya Kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya.
#bazil Mjungu.
#bazotvnews.
Comments
Post a Comment