MTATURU NI SAHIHI SINGIDA MASHARIKI
Na OMARY GWATY
0652162605
MH,MIRAJI MTATURU, Mbunge ingizo jipya la Singida Mashariki ni kiongozi anayeshughulika na shida za watu moja kwa moja,huyu hayupo kwenye Siasa za Maji taka,kwake fikra zake ni kuwapigania wananchi wake wapate Huduma zote wanazostahili!
Hakuna jambo hata Moja ambalo huwa analifanya njee ya mipango. Kiufupi huyu kiongozi ana Vission yake inayomwongoza.
Kiini cha Kazi zake ni kutengeneza mambo mapya, kuleta idea Mpya, Kufikiri katika Miaka zaidi ya Kumi Ijayo.
Utofauti wake mkubwa na viongozi waliopita ni kwamba hana Siasa za majigambo na matusi,chuki nk.huyu ni mstaarabu anayeamini katika Maendeleo kwa wote bila kujali itikadi ya chama,haya yalionekana akiwa DC wa Ikungi!
Tofauti nyingine ni kuwa wakati viongozi wengine walikuwa wakiamka asubuhi wanafikiria ni wapi kwenye kero ya maji, Ardhi nk wakaweke maspika na kuanza kuhutubia kwa kudai kuwa wanasikiliza kero za wananchi.....,
MH MTATURU yeye huwa anatengeneza Mipango Mipya ya Utekelezaji, Swala la Kuzurura na maspika sijawahi kuona kwa kipindi ambacho alikuwa DC wa Ikungi!
Kuna hatari kubwa sana kama Kiongozi atakuwa ni matatizo "oriented" yaani kiongozi anayewaza kusikiliza Kero tu kuanzia January hadi December huyu hatoweza kuleta Tanzania mpya.
Mh,Mtaturu kupitia cheo chake cha DC Ikungi amefanikiwa kuhamasisha wananchi kufanya Maendeleo katika wilaya yake kwani mashule,hospital karibu kata zote zimejengwa!
Wananchi wa Singida Mashariki wamepata muwakilishi sahihi anayeendana na kasi ya Mheshimiwa Rais na ameshawasilisha kero ya Maji bungeni!
Wananchi na viongozi wote wa Singida Mashariki tuache Siasa za chuki tumuunge mkono Mtaturu Singida Mashariki Itapaa ndani ya muda mfupi!
SINGIDA MASHARIKI
UONGOZI WENYE MAONO!
Comments
Post a Comment