MTATURU AITAKA SERIKALI KUJENGA SOKO LA KISASA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA IKUNGI


na Bazil Mjungu: Dodoma
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itatenga fedha kwa ajili ya kujenga soko la kisasa wilayani Ikungi Mkoani Singida.

Mtaturu ameuliza swali hilo April 24,2023, Bungeni Jijini Dodoma.


Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dr Festo Dugange amesema Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imeweka mpango wa kujenga soko la kisasa katika Kijiji cha Ikungi lenye ukubwa wa Ekari 2.

Amesema kwa sasa Halmashauri inaendelea kufanya mazungumzo na wananchi ambao wamejenga vibanda vya biashara katika eneo hilo lililoainishwa na mipango miji kwa ujenzi wa soko la kisasa.

"Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na UN WOMEN imekamilisha ujenzi wa jengo la mabucha na mbogamboga lenye thamani ya shilingi Milioni 82 katika eneo hilo,"amesema.

Aidha, ameahidi kuwa serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa soko la kisasa Ikungi.

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida