ZIARA YA DC APSON, IKUNGI YAZIDI KUTATUA KERO, KUZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson amewataka wakandarasi kuzingatia ubora katika ujenzi wa miundombinu ya Serikali ili kuendana na wakati...

Akizungumza mara baada ya kutembela Miradi mbalimbali leo tarehe 05 April 2023 ikiwemo shule ya Sekondari Mwau katika ujenzi wa maabara mbili za Kemia na biolojia zitakazogharimu Milioni 118.1,shule ya msingi Mwau katika ujenzi wa vyoo unalio fadhiliwa na Shanta Gold mine matundu 17 yaliyogharimu milion 46 pamoja na Zahanati ya Mang'onyi iliyogharimu Shilingi milioni 144.8 Mkuu wa Wilaya amewapongeza kwa hatua nzuri waliyoifikia na kushauri majengo yazingatie maagizo yanayotolewa na serikali...

"Majengo lazima yawe yakisasa ili mtoto aweze kusoma katika mazingira yanayomvutia kuanzia sakafu,madirisha,rangi hata mabati yawe yakisasa."alisema Mkuu huyo wa Wilaya ilaya...


Kwa upande mwingine aliwapongeza Mgodi wa Shanta kwa kufadhili mradi wa vyoo pamoja na Zahanati ya Mang'onyi kwa kukamilika katika ubora na kuwaomba kuendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali za Maendeleo...

Aidha, katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya alizindua Vyoo vya shule ya Msingi Mwau kuanza kutumika rasmi na kuwataka wanafunzi kuzingatia usafi na kuvitunza vyoo hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu.

Sambamba na ziara hiyo iliambatana na uongozi wa Shanta Gold Mine ambapo mkuu wa Wilaya alitembelea mgodi huo kuona maendeleo ya shughuli mbalimbali zinazofanyika mgodini hapo.

#bazotvonline
@bazotvnews

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida