SHIRIKA LA RESTLESS DEVELOPMENT TANZANIA LAWAFUNGULIA NJIA VIJANA WAJASIRIAMALI MKOANI SINGIDA.

Na Bazil Mjungu Singida.
Shirika la Restless Development Tanzania likiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bi. Haika, Meneja wa Miradi Bw. Ridhione Juma na Afisa mawasiliano wa shirika hilo wakiambatana na Saimon Sirilo Mratibu wa Vikundi vya Ujasiriamali kwa vijana Mkoa wa Singida.

Wamewatembelea Vijana walionufaika na mafunzo ya Ujasiriamali yaliyotolewa na Shirika Hilo.


Wilaya ya Ikungi na Itigi Mkoani humo Vijana wa Vikundi vya Ufugaji Nguruwe wa kisasa kutoka Mwisi, Kikundi cha Chaki kilichopo Mwisi, Kikundi cha Tofali Cha Puma na kikundi cha Tofali Ikungi.


Vijana hao wamekiri kunufaika na mafunzo hayo na kusema mafunzo hayo yamewasaidia kufika mahali kwa kuanzisha Vikundi, kusajili na kupata Mikopo kutoka Halmashauri wanazo ishi.

Aidha, Shirika limewasaidia Fedhaza chakula na usafiri uliowawezesha kushiriki kikamilifu mafunzo hayo.


Uongozi wa shirika umewapongeza Viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata na Halmashauri kwa kushikamana na shirika hilo toka mwanzo hadi mwisho wa mafunzo

Shirika limetoa Shukrani Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Halmashauri ya Itigi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mue. Jerry Muro, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Bi. Haika Massawe Pamoja na Maafisa wote wa kata zilizoshiriki na Watumishi wa Halmashauri ya Itigi Afisa maendeleo Be. Fred na Maafisa maendeleo wote wa Kata.



Bazil Mjungu
#BazotvNews.



Comments

  1. Very nice, it is exciting to work with restless Development

    ReplyDelete
  2. Hakika Restless Development ni shirika linalotuwezesha vijana kutambua umuhimu wetu vijana katika maendeleo yetu na taifa kwa ujumla.. hongera sana RD

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida