FUNGUO SABA ZA KUKUZA KIWANGO CHAKO NA MUNGU ( SEVEN KEY TO RAISE YOUR PERSONAL LEVEL WITH GOD.)
Kitabu cha Yoshua 1:8
8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Tunachokiona hapa ni msisitizo wa Mungu kumsisitiza Nabii Joshua juu ya kulitafakari NENO la Mungu, Usiku Na Mchana.
Kusudi la Waraka huu Au Ujumbe huu ni kutusaidia sisi wasomaji kujua nini ni lazima katika Maisha yetu Na wala sio ombi kwamba Tusome Na kulitafakari Neno la Mungu Usiku Na mchana.
Tafsiri yake hapa juu ya NENO la MUNGU kwa ufupi ni kwamba ni Jumla ya Mawazo ya Mungu juu ya Mwanadamu.
➡️Ndani ya NENO la Mungu kuna Maamuzi ,( Hukumu) sheria. Maaagizo Na Njia za Mungu za kumtoa mwanadamu katika Shida aliyonayo Na kila Aina ya changamoto anayopitia Ili kumfanikisha katika mambo yote Na kukusaidia katika mambo yote ili kuishi la kulishika shauri lake ( kusudi la Bwana.)
Sababu hizo ni
1️⃣Uweze kuelewa nini Mawazo ya Mungu juu ya Maisha yako.
➡️ Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
⁃ Ili uweze kujua Kila siku Mungu anakuwazia nini Ni Muhimu kusoma NENO lake Na kulitafakari Neno la Mungu Ili likupe kuelewa juu ya Kazi zako, Biashara zako Na Huduma yako Na Maono yako kuhusu success .
2️⃣Upate Kufanikisha Njia yako
Zaburi 32:8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
➡️Ni Mungu Tu pekee ndiye anayemwambia Nabii Joshua kwamba nitaifanikisha njia yako.Joshua 1: 8b tukumbuke kila moja ana namna ya njia yake juu ya kulitumikia shauri la Bwana. Na mafanikio sasa yanatajwa katika kulisoma Neno la Mungu Na kulitafakari kwa sababu Neno la Mungu ni taa ya miguu yangu.
Zaburi 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.
3️⃣Neno linatusaidia tumtende Mungu dhambi.
Zaburi 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Kwa kadri unavyotunza Neno ndani ya Moyo wako kwa Undani zaid Na meditation yake kwa Upana zaid Ndivyo linavyokusaidia Na kukulinda Ili usitende dhambi.
➡️Neno hilo litakuonyesha hila Na mitego na mbinu za Ibilisi shetani.
Pia hilo Neno litakupa Ushindi Na vishawishi juu ya ADUI shetani.
4️⃣Neno litakufanya UKue Na Kuongezeka KIIMANI.
Warumi 10:17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Ikiwa chanzo cha Imani huja kwa kusikia Na kusikia huja kwa Neno la KRISTO basi maana yake kwa kadri unavyolisoma Neno la kulitafakari kisha ukajitamkia Na kujinenea Ili Mpaka ujisikie Moyoni kwamba umeshinda kwa Imani.
5️⃣Neno la Mungu limebeba jibu la mahitaji yako.
Zaburi 107:20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.
➡️kwa kuwa ndani ya Neno kuna Mawazo Na Mawazo mikakati na njia ya kukufanikisha ki Maisha , unapolitafakari sio tu utaelewa Mipango ya Mungu juu ya Maisha yako pia litakupa Njia ya kujikwamua katika changamoto mbalimbali za ki Maisha , KIROHO Na KIMWILI.
6️⃣Neno la Mungu litakupa kustawi sana.
Joshua 1:8b Anasema Ili Uweze kustawi sana
➡️Biblia inapozungumzia juu ya kustawi sana ina maanisha ni kulawala na kumiliki vema .Mtu ambaye ndani yake amejaa Neno la Mungu kwa Wingi ndani yake huyo ana Uwezo mkubwa wa kuwa Na Kibali cha
Kutawala , Kumiliki Na Kuongoza watu pia.
7️⃣Neno litakupa Miaka Mingi Duniani
➡️ Mithali 3:1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Mithali 3:2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
8️⃣Neno la Mungu litakufanya uwafumdishe wengine kumjua Yeye.
KUMBUKUMBU LA TORATI 6
Amri kuu
1Na hii ndiyo sheria, amri na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayovuka kuimiliki; 2 upate kumcha BWANA, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. 3Sikiliza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali.
4 Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja 5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
➡️Mungu anataka watu wote wamjue yeye focus yake ni kwamba utakaposoma Neno lake akajifunua kwako basi anatamani ushiriki kutangaza Ukuu wake kwa kila hali Na Mali Ili kuwakumbusha wengine wasimsahau yeye peke yake.
#bazotvNews
Comments
Post a Comment