Posts

Showing posts from October, 2018

TATIZO LA MAFUTA IKUNGI KUISHA

Image
Leo tarehe 30 Octoba,2018  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amekagua ujenzi wa kituo cha mafuta kinachojengwa Makao Makuu ya Wilaya. Huduma ya mafuta ni changamoto kubwa Kwenye uendeshaji wa shughuli za kila siku za Serikali na watu binafsi ikiwemo Huduma za usafirishaji abiria, Inatulazimu kwenda km 40 hadi Singida mjini kupata Huduma ya mafuta. Dc mtaturu amemshukuru sana ndugu Farid Bazaar kukubali ombi la wilaya la  kuwekeza kwa kujenga kituo cha mafuta na matarajio kianze kutoa Huduma mwishoni mwa Novemba 2018. Aidha DC Mtaturu ameongeza kwa kusema, Wananchi wanapaswa kuelewa maana ya uwekezaji ili kuwapa ushirikiano na kuleta huduma kwa wananchi, "Kwa wilaya yetu Mara nyingi wanapotokea   wawekezaji wamekua hawapewi ushirikiano na kusababisha mitafaruku kati ya wamiliki  wa maeneo na mwekezaji na kuwafanya wawekezaji kuogopa kuja kuwekeza katika wilaya yetu kitu ambacho kimetufanya kuwaelekeza wananchi kuelewa maana ya neno mwekezaji" Hakika uongozi

IKUNGI. WANANCHI WAMPONGEZA DC MTATURU KUWA DC WA KWANZA KUFIKA KUFANYA ZIARA KIJIJINI KWAO TANGU UHURU

Image
Wanan chi wamempongeza Mhe. Miraji Mtaturu kwa kuwa DC wa kwanza kufanya ziara kwenye vijiji vyao toka Uhuru.  Vijiji vya Kipunda na Masweya  wanajenga zahanati zipo hatua za lenta na Hanamu. DC Mtaturu amewapongeza wananchi kwa jitihada hizo na kuwataka waongeze bidii na serikali itaendelea kuwaunga mkono, Aidha amewaahidi kuwachangia bati 100 zahanati ya Songandogo na kutoa kibali wapasue mbao za kupaua ili mapema february 2019 huduma ianze kutolewa. DC Mtaturu ameongeza kwa kuwasisitiza uhifadhi mazingira na kupanda miti kila kaya 10 na vijiji vitenge hekari 10 kama msitu kisiwa. Wananchi wameelekezwa kufuata kalenda ya msimu wa kilimo ili kujihakikishia uzalishaji wa chakula cha kutosha msimu huu. Aidha. Maafisa Ugani wameelekezwa kuwafundisha wakulima viongozi kwenye vitongoji ili wawasaidie wakulima wenzao kujua kanuni bora za kilimo. DC Mtaturu kupitia mkutano huo amewahikikishia wananchi serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha huduma zot

IKUNGI. SERIKALI KUCHIMBA VISIMA VYA MAJI KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI

Image
Ziara DC Ikungi Day 3: Tumeendelea kuwafikia wananchi kukagua miradi na kuhamasisha maendeleo Vijiji vya Damankia na Samaka. Maagizo/Utatuzi changamoto na Pongezi;  1.Wananchi wamelalamikia Uongozi wa kijiji cha Damankia kutowasomea mapato na matumizi na kudhoofisha maendeleo ya kijiji ikiwemo maendeleo ya shule,DC Mtaturu amemwagiza DED aitishe mkutano wa wananchi wote kujadili changamoto hiyo kufikia tarehe 30 Octoba. 2.Miradi ya kijiji cha Samaka;Ofisi ya Serikali kijiji na Ujenzi wa Matundu 12 ya Choo Shule ya msingi wananchi wamefyatua matofali 9000. DC amewaunga mkono wananchi matofali 500 na saruji mifuko 20 kusaidia kumalizia ujenzi wa Ofisi ya Kijiji,Mabati 30 kupaua matundu 12 ya Vyoo,magoli ya chuma kwenye uwanja wa mpira na mipira miwili kwa ajili ya wanafunzi. 3.Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto DC Mtaturu ameagiza wakati mpango wa  ujenzi wa zahanati DED alete wauguzi mara moja kwa mwezi Samaka kliniki kwa ajili ya akina mama na watoto kuwapunguzia umbali kwenda Dung'un

TEKELEZA WAJIBU WAKO IKUNGI IENDELEE

Image
DC Mtaturu atoa maagizo kwa watumishi ikiwa ni MPANGO KAZI . Maagizo: 1.Viongozi watoke ofisini kusikiliza na kutatua kero za Wananchi. 2.Kusoma mapato na matumizi kwa mujibu wa sheria. 3.Kusimamia uhifadhi wa mazingira. 4.Msimu wa kilimo2018/19 idara ya Kilimo kuandaa kalenda maalum kwenda na mpango mkakati wa idara ikiwemo kutumia zana bora za kilimo na mbegu bora. 5.Jamii kushiriki kusimamia Elimu kwa kusaidiana na Wataalam wa Idara husika ili kuongeza Ufaulu. 6.Kampeni ya Usafi wa mazingira,Ujenzi wa Vyoo Bora na Unawaji mikono. "IkungiYetuSote#TuijengePamoja#

MAAZIMISHO YA NYERERE DAY IKUNGI SINGIDA

Image
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe MIRAJI JUMANNE MTATURU kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ikungi, Wameshiriki kufanya usafi katika Hospital teule ya Wilaya ya Ikungi ambayo ni Makiungu Hospitali,  Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere. SR, Dkt. MAGDALENE UMOREN. Mganga mkuu Hospitali teule ya wilaya, akitoa shukrani kwa ugeni uluojitokeza Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Kwa kufanya usafi na kutoa zawadi kwa wagonjwa na wazazi. Padre. MARTIN SUMBI. Afisa Utawala wa Hospitali ya Makiungu, Akiishukuru Ofisi ya Mkuu wa wilaya na ya Mkurugenzi wa ushirikiano walioutoa Leo katika kufanya usafi na kutoa zawadi kwa wazazi na wagonjwa  Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu. Akiwashukuru watumishi wa Halmashauri na watumishi wa Hospital ya Makiungu kwa ushirikiano waliouonyesha katika kufanya usafi kwa pamoja na kuwatembelea wagojwa  Siku ya

DC Mtaturu. Chuo cha VETA kujengwa Ikungi.

Image
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Amewataka wazazi kuwahimiza wanafunzi kuhudhuria vizuri katika masomo ili kuleta ufaulu mzuri katika wilaya ya Ikungi na Mkoa kwa ujumla. Akihutubia kwenye mahafali ya kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Siuyu, Mtaturu amewaomba wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuhakikisha kwa pamoja wanatokomeza utoro usio wa lazima kwa wanafunzi,  Aidha, DC Mtaturu akasema " kutokana na ufaulu unaonyesha 20% tu ya wanafunzi ndio hufaulu kujiunga na vyuo ama kidato cha tano, na kubakiza 80% ya waliofeli masomo na kubaki nyumbani wakiwa hawana chochote cha Serikali ya wilaya ya Ikungi imeamua kujenga chuo cha Veta ili wanao baki hawa 80% wajiunge na chuo hicho na itafanya wapate fani mbalimbali ili kujikimu katika maisha yao" Mwisho akawataka walimu kujituma zaidi ili kuongeza ufaulu wa shule hiyo.

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida

Image
* IKUNGI *Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amezindua Jengo la Kituo cha Huduma ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Matare Ikungi Jengo lililotumia zaidi ya Milioni 230, Katika uzinduzi huo, Mhe Mtaturu amewataka watumishi wa Afya kutoa Huduma ya Mama na Mtoto kwa moyo wa HURUMA ili kuwafanya wananchi kuiamini Serikali waliyoichagua inayo ongozwa na Kipenzi cha watu Dkt John Pombe Magufuli, Aidha amewataka Wananchi kulipia bima za Afya ili kujiwekea akiba ya matibabu kwani maradhi hayana maandalizi. Alimaliza kwa Kumuagiza Mganga Mkuu wa wilaya kuhakikisha dawa hazikosekani katika zahanati zote na vituo vya Afya wilayani Ikungi.*