MTU WA WATU, KINARA WA MAENDELEO SINGIDA MASHARIKI Mh. MIRAJI JUMANNE MTATURU OCTOBER 22, 2022 AMESHIRIKI MAHAFALI YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA MSINGI NG'ONGOSORO KATA YA ISSUNA JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI WILAYA YA IKUNGI.

Katika Risala ya wanafunzi shuleni hapo imeeleza mafanikio na changamoto za shule yao ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu, walimu na vifaa vya stationary kwa ajali ya kuandaa mtihani ikiwemo computer, printer na photocopy machine.

Diwan wa kata Issuna Mh Stephano Missai alimshukuru Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki mhe Miraji Mtaturu kwa kuwasemea matatizo waliyonayo bungeni na Serikali kuwaletea fedha za Miradi ya maendeleo kama sasa Isuuna tumeona madarasa yamejengwa Sekondari ya issuna, jengo la utawala na jengo la maabara limekamilika. 

Tumepata fedha zaidi ya 70m kumalizia zahanati ya Issuna na huduma zimeanza kutolewa ambapo ilikuwa kero ya muda mrefu sana wananchi kufuata huduma za afya  kijiji cha Nkuhi au Ikungi kilomita zaidi ya 35.


Pia mtendaji wa kijiji cha Ng'ongosoro amemshukuru Mbunge kwa kuwaletea 4m kusaidia ujenzi unaendelea wa madarasa mawili kwa sasa wamenunua mifuko 150 ya saruji wameanza kufyatua matofali waanze ujenzi na wananchi wanashiriki kuleta mchanga na maji.


Naye Mh Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Miraji Jumanne Mtaturu katika salamu ya  hotuba yake  aliwapongeza sana Jumuiya ya shule ya msingi Ng'ongosoro kwa maendeleo ya taaluma na kuifanya shule yao kuwa miongoni mwa shule kumi bora kitaaluma wilaya ya ikungi.

Amechukua fursa hiyo kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu, Afya, Miundombinu ya Barabara, Umeme  na Maji.

Mh mbunge alisema wilaya Ikungi ilipatiwa jumla ya 2.6 bilioni tukajenga madarasa 67, na  kwa kata ya Issuna mlipatiwa 60m na mkajenga madarasa matatu .

Wiki iliyopita tumeletewa 560m kwa ajili ya madarasa 29 na tumepatiwa 40m kwa ajili ya madarasa mawili. 

Mh mbunge aliendelea kusema...

 "Ninawakikishia Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya elimu ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia na ushihidi ndio huu unaonekana dhahiri". alisema mh  mbunge.

Amewahidi kuwaleta wataalamu wa kuja kufanya utafiti wa  chanzo cha maji ili kumaliza tatizo la maji hapo shuleni,
 pia kuwaletea Computer 2, Printer 1 na Solar vyote vikiwa na thamani ya Tsh 6.5m.

Katika kuimaimarisha michezo shuleni hapo Mh mbunge ametoa jezi na mipira kwa ajili ya michezo shuleni hapo katika juhudi za kukuza vipaji pamoja na kuwa sehemu ya kukuza taaluma.

 Amewashukuru viongozi wa Dini kwa kuendelea kuliombea Taifa Amani.

Kwa kuitimisha hotuba yake Mh mbunge huyo amewahimiza wananchi kuendelea kushikamani na kuwa sehemu ya kutekeleza  miradi ya maendeleo kwani inaletwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote bila kujali mitazamo au itikadi zao.

*Imetolewa na ofisi*
*ya Mbunge wa* *Jimbo la Singida* *Mashariki*
*Mh Miraji Jumanne Mtaturu*
*Leo October 23,2022.*

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida