CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA IKUNGI B LAFANYA UCHAGUZI
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Kimeendelea na zoezi la kuimarisha Chama hicho ambapo wamefanya Uchaguzi katika ngazi ya Tawi katika Tawi la Ikungi B ambapo wamefanya uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti iliyokuwa na wagombea watatu akiwemo Ndugu Shabani Kisuda, Ally Ndoghwe na Hashimu Hasan. Wapiga kura waliojotokeza ni 74 ambapo Katika uchaguzi huo Ndugu Kisufa Aliyekua akishikilia kiti hicho alifanikiwa kutetea nafasi yake kwa kupata kura 66 na wenzake kila mmoja akiambulia kura mbili kila mmoja na kura nyingine ki.
Tawi lililofanya uchaguzi ndilo linalobeba makao makuu ya Chama Wilaya ya Ikungi na makao makuu ya Wilaya, Mwenyekiti wa Uchaguzi huo Alhaji Salum Chima alitoa maelekezo mbali mbali ya uchaguzi na kumhimiza Utendaji uliobora Katika Chama na kuwashukuru wanachama waliojitokeza kushiki Katika uchaguzi huo.
Katika uchaguzi huo Walifanikiwa kushiriki Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya akiwemo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi nduugu Stamil Omar Dendego, Katibu wa Jumuiya ya wazazi Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi ndugu Hawa mjumbe wa mkutano mkuu Taifa wilaya Ndugu Kulwa Shilinde.
Wajumbe 10 wa Halmashauri ya tawi na watano wa mkutano mkuu wa Kata na mwakalishi wa mkutano mkuu wa Wilaya pia walichaguliwa.
Katika kuwakabidhi Uongozi mpya Mwenyekiti huyo wa Uchaguzi aliwaagiza waweke malengo makuu katika kipindi chao cha miaka mitano kama ifuatavyo 1. Wajenge ofisi bora ya Tawi ya chama na washirikiane na Serikali ya kijiji kutafuta eneo la kujenga shule ya msingi ili kupunguza adha ya Uhaba wa Shule za Msingi Katika Kijiji hicho.
Comments
Post a Comment