Posts

Showing posts from 2022

MASHINDANO YA MPIRA WA WAVU YA MAVUNDE CUP YAZINDULIWA RASMI LEO JIJINI DODOMA

Image
Na Mwandishi wetu Dodoma: Mashindano ya mpira wa wavu maarufu kama * MAVUNDE CUP * yamezinduliwa rasmi leo katika shule ya Msingi Mlezi Jijini Dodoma huku yakijumuisha Timu 18 za wanaume na wanawake kutoka mkoani Dodoma na nje ya Dodoma. Mashindano hayo yamezinduliwa leo na Diwani wa Kata ya Hazina * Mh. Samwel Mziba * akiongozana na Diwani wa Viti Maalum * Mh. Flora Lyacho * huku wote wakitoa rai kwa Vijana wa Dodoma kuchukua fursa ya haya mashindano kama sehemu ya kuendeleza na kukuza vipaji vyao. Aidha zoezi hili la uzinduzi wa mashindano limekwenda sambamba na ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu zote zinazoshiriki katika mashindano hayo pamoja na ukarabati wa kiwanja cha kuchezea. Mashindano hayo yatafikia tamati tarehe * 01.01.2023 * siku ya Jumapili, ambapo Mgeni Rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa * Mh. Anthony Mavunde * Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Mfadhili wa mashindano hayo. #bazotvnews.

DARASA NA STREETLECTURE UTAJIRI na UMASIKINI

Image
Na Shaabani Y. Shaabani : Utajiri haimaanishi kuwa na akaunti ya benki nono. Utajiri kimsingi ni uwezo wa kutengeneza mali. Mfano: Mtu anayeshinda bahati nasibu au kamari. Hata akishinda milioni 100 si tajiri: Ni maskini mwenye pesa nyingi. Ndiyo sababu 90% ya mamilionea wa bahati nasibu wanakuwa maskini tena baada ya miaka 5. Pia una matajiri ambao hawana pesa. Mfano:Wajasiriamali wengi. TAYARI wapo njiani kuelekea kwenye utajiri japokuwa hawana pesa, maana wanakuza akili zao za fedha na huo ndio utajiri. * Tajiri na maskini wanatofauti gani? * Kwa maneno rahisi: Tajiri anaweza kufa ili kuwa tajiri na hutumia mda wake mwingi kujigunza na na ya kupiga hatua zaidi, Na maskini anaweza kuua ili kuwa tajiri na hutumia mda wake mwingi kusengenya,kueneza chuki,Ubinafsi na Kuwaza Uwasherati. Ukiona kijana anaamua kufundisha, kujifunza mambo mapya, ambaye anajaribu kujiboresha mara kwa mara, ujue kwamba yeye ni tajiri. Ukiona kijana anafikiri kuwa tatizo ni serikali, na anayedhani ku

MTATURU ATAHADHARISHA KANUNI ZA SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI.

Image
Na Bazil Mjungu Dodoma: MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (CCM), Mhe. Miraji Mtaturu, ametahadharisha kanuni zitakazotungwa kwenye muswada wa sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi wa mwaka 2022  kuhakikisha zinaendana na sheria ili zisiibue malalamiko kwa wananchi. Akichangia leo bungeni, Mtaturu amesema sheria hiyo ni nzuri lakini utungaji wa kanuni hizo uendane na sheria iliyopitishwa. “ Pamoja na sheria hii kuwa nzuri na tumekuwa tukipitisha hapa, kumekuwa na changamoto ya kanuni, niombe sana kwenye eneo hili na sisi tunamuamini Waziri, sheria ikitungwa nzuri iende hivyo hivyo na kanuni ziwe nzuri,” amesema Mtaturu. Mtaturu amesema eneo la utungaji wa kanuni linaweza kuwa mwiba mwingine katika utekelezaji wa sheria zinazopitishwa na bunge. “ Tumekuwa tukipitisha baadhi ya sheria lakini ile nafasi ya kutengeneza kanuni huwa inakwenda kuharibu kabisa sheria, matokeo yake wabunge tunaulizwa mlipitishaji sheria hii, kumbe kanuni imekwenda kuharibu kabisa maudhui mazima ya sheria ambayo

MTU WA WATU, KINARA WA MAENDELEO SINGIDA MASHARIKI Mh. MIRAJI JUMANNE MTATURU OCTOBER 22, 2022 AMESHIRIKI MAHAFALI YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA MSINGI NG'ONGOSORO KATA YA ISSUNA JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI WILAYA YA IKUNGI.

Image
Katika Risala ya wanafunzi shuleni hapo imeeleza mafanikio na changamoto za shule yao ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu, walimu na vifaa vya stationary kwa ajali ya kuandaa mtihani ikiwemo computer, printer na photocopy machine. Diwan wa kata Issuna Mh Stephano Missai alimshukuru Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki mhe Miraji Mtaturu kwa kuwasemea matatizo waliyonayo bungeni na Serikali kuwaletea fedha za Miradi ya maendeleo kama sasa Isuuna tumeona madarasa yamejengwa Sekondari ya issuna, jengo la utawala na jengo la maabara limekamilika.  Tumepata fedha zaidi ya 70m kumalizia zahanati ya Issuna na huduma zimeanza kutolewa ambapo ilikuwa kero ya muda mrefu sana wananchi kufuata huduma za afya  kijiji cha Nkuhi au Ikungi kilomita zaidi ya 35. Pia mtendaji wa kijiji cha Ng'ongosoro amemshukuru Mbunge kwa kuwaletea 4m kusaidia ujenzi unaendelea wa madarasa mawili kwa sasa wamenunua mifuko 150 ya saruji wameanza kufyatua matofali waanze ujenzi

MAGAZETINI: MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 14, 2022 MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 14, 2022

Image
MAGAZETINI leo October 14, 2022 #bazotvonline @bazotvnews

MAGAZETINI: MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 14, 2022 MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 14, 2022

Image
MAGAZETINI leo October 14, 2022 #bazotvonline @bazotvnews

MAKALA YA WIKI LA VIJANA MKOANI KAGERA PAMOJA NA KILELE CHA KUZIMA MWENGE WA UHURU MWAKA 2022

Image
Na Simon Sirilo: Kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development  linalofanya kazi na Vijana tumeshiriki katika maadhimisho ya wiki la vijana na kuweza kubadilishana mawazo na vijana wengi wa Kitanzania mkoani kagera kwa kuwajengea uwezo katika mambo kadhaa ikiwemo namna ya kujiajiri,Afya na makuzi pia. Kupitia mambo mtambuka yanayowahusu kujenga uchumi wa vijana nilifanikiwa kuwa moja ya wanajopo walioendesha mdahalo uliojikita katika kuzungumzia hatma ya uchumi wa vijana kupitia mafaniko,changamoto na mapendekezo kwa serikali. Binafsi,nilitoa mawazo yangu kama ifuatavyo 1:Vijana kuwa na uthubutu na kuanzisha mambo/miradi japo kwa kidogo ili kuweza kuiaminisha serikali kuwa vijana tunao uwezo,maarifa,nguvu na ari ya kufanya kazi...hapa ndipo serikali itawashika mikono kupitia zile fedha asilimia 4 za vijana kutoka halmashauri. Uthubutu huleta kuaminika zaidi kuliko maneno matupu,kijana mwenye uthubutu huaminika zaidi kuliko asiyeanza kabisa. 2: Vijana tujitahidi kutafsiri  fursa z

WAZEE IKUNGI WAKUTANA NA DC MURO

Image
Na Mathew Anton Singida. Ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya wazee Duniani ambayo kimkoa maadhimisho yatafanyika katika Wilaya ya Ikungi, baadhi ya wazee wamekutana na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho yatakayifanyika kesho tarehe 01/10/2022 Wakizungumza ofisini kwa Dc Muro wazee hao wameishukuru serikali ya wilaya kwa namna inavyoshughulikia kero na changamoto zinazowakumba wazee na kumuhakikisha Dc Muro kuwa kesho wana jambo la kusema kwa Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan Katika mazungumzo hayo Dc Muro amewahakikisha wazee kuwa serikali itaendelea kuondoa kero na changamoto zinazowakumba wazee ikiwemo kuweka mfumo endelevu wa kuhakikisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya wilaya, kata na vijijini yanafanya kazi ipasavyo hatua itakayowawezesha wazee wenyewe kutatua changamoto ndogondogo zinazowakabili wakati serikali ikiendelea kutatua kero mtambuka za wazee.

ASKOFU AFARIKI DUNIA AKIHUBIRI IBADA YA MAZISHI MKOANI TAANGA

Image
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa George Chiteto amefariki dunia jana mchana mara baada ya kumaliza kuhubiri katika mazishi ya mke wa Askofu Lugendo wa Dayosisi ya Mbeya Bi. Hilda Lugendo yaliyofanyika wilayani Muheza mkoani Tanga. Tukio hilo la huzuni limekuja ghafla mara baada ya kumaliza mahubiri katika msiba huo, Askofu George Chiteto alirudi kukaa kwenye kiti ili taratibu zingine za ibada ziendelee, alianza kujisikia vibaya, akaishiwa nguvu kisha kupoteza fahamu. Utaratibu wa kumkimbiza hospitali ulifanyika haraka na kufikishwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza Tanga na saa chache akaaga dunia. Askofu George aliwekwa wakfu Jumapili iliyopita Agosti 28, 2022 kuwa Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma na Septemba 03, 2022 akawa ameaga dunia akihudumu nafasi hiyo ya uaskofu wa Dayosisi hiyo kwa takribani siku kati ya tano tu. Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, aliyekuwepo katika ibada hiyo ya mazis

CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA IKUNGI B LAFANYA UCHAGUZI

Image
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Kimeendelea na zoezi la kuimarisha Chama hicho ambapo wamefanya Uchaguzi katika ngazi ya Tawi katika Tawi la Ikungi B ambapo wamefanya uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti iliyokuwa na wagombea watatu akiwemo Ndugu Shabani Kisuda, Ally Ndoghwe na Hashimu Hasan. Wapiga kura waliojotokeza ni 74 ambapo Katika uchaguzi huo Ndugu Kisufa Aliyekua akishikilia kiti hicho alifanikiwa kutetea nafasi yake kwa kupata kura 66 na wenzake kila mmoja akiambulia kura mbili kila mmoja na kura nyingine ki. Tawi lililofanya uchaguzi ndilo linalobeba makao makuu ya Chama Wilaya ya Ikungi na makao makuu ya Wilaya, Mwenyekiti wa Uchaguzi huo Alhaji Salum Chima alitoa maelekezo mbali mbali ya uchaguzi na kumhimiza Utendaji uliobora Katika Chama na kuwashukuru wanachama waliojitokeza kushiki Katika uchaguzi huo. Katika uchaguzi huo Walifanikiwa kushiriki Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya akiwemo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi nduugu

MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA MUUNGANO YAFANA MKOANI SINGIDA

Image
Na Bazil Mjungu _ Ikungi Singida Mkuu wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro ameongoza maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na zanzibar kwa kufungua kongamano la vijana mkoa wa Singida kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Binilith S. Mahenge Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano ya chuo cha uhasibu singida ambapo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo umuhimu wa kudumisha muungano, fursa za uchumi katika mkoa wa singida na ushiriki wa vijana katika sensa ya watu na makazi Akizungumza katika kongamano hilo Dc Muro amesema Tanzania Bara haiwezi kuwa salama kama Tanzania zanzibar haitakuwa salama kiulinzi, kiuchumi na kijamii Amesema wakati dunia ikiungana katika muktadha mbalimbali ni vizuri kwa Tanzania kudumisha muungano wao ili kutoa nguvu ya kuleta maendeleo kwa jamii za pande zote mbili Akihitimisha hotuba yake amewataka vijana kushirikiana kikamilifu na viongozi wa serikali katika kuhakikisha jamii inashiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayotar

MSAADA UNAHITAJIKA KUMALIZIA MSIKITI: BAJETI YA KUMALIZIA MSIKITI UNYANGWE.

Image
Kushoto mwa MSIKITI. Kulia mwa Msikiti. Mbele ya Msikiti. 1. Nondo za Nguzo za Katikati 100 = 19,000 X 100 = 1,900,000/= 2. Mbao za Kenchi 164 X = 11,000 X 164 = 1,804,000/= 3. Mbao za kupaulia 189 = 7000 X 189 = 1,323,000/= 4. Mbao za Fisha bord 30 = 25000 X 30 = 900,000/= 5. Mabati 276 = 26,000 X 276 = 7,176,000/= 6. Misumari ya bati kilo 50 = 6000 X 50 = 300,000/= 7. Misumari ya mbao kilo 50 = 6000 X 50 = 300,000/= 8. Madirisha 10. Aluminium = 450,000 X 10 = 4500,000/= UFUNDI 1,800,000/= Jumla Milioni 19,983000 Bazl Rajabu Mjungu.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 3/2022

Image
Magazateni leo: Januari 03/2022