SHANTA GOLD YAPATA PONGEZI KUSIMAMIA LOCAL CONTENT
Na Mwandishi wetu Singida: Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ameeleza kuwa, Mgodi Mpya wa Kati wa Dhahabu wa Shanta ndio Mgodi pekee Tanzania unaotekeleza ipasavyo Matakwa ya Sheria ya matumizi kwa Jamii husika (Local Content). Amesema hayo tarehe 30 Julai, 2021 baada ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Mgodi wa Kati wa Dhahabu wa Shanta Singida (SINGIDA GOLD MINE) ambao upo Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida. Amesema historia ya ujenzi wa Mgodi huo, kwa miaka mitano yote iliyopita Mgodi wa Shanta ndio Mgodi wa Kati mpya uliojengwa hapa Nchini kwa muda mfupi. Akizungumzia kuhusu umuhimu wa Sheria ya Local content Waziri Biteko amesema katika uwekezaji inawahitaji Wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo ili kufanya uchumi uwe na maana. “Kama biashara wafanye wenyeji, tulikuwa na Migodi ambayo hata nyama ilitoka South Africa, lakini Mgodi ambao mwaka huu tumewapa tuzo ya Local content, huu ndio mgodi ambao asilimia 100 ya walioajiriwa ni watanzania" ameeleza Biteko. Aidha, am