Posts

Showing posts from May, 2020

MTATURU AKUTANA NA BODABODA JIMBONI KWAKE KUSIKILIZA KERO NA KUZIPATIA UFUMBUZI

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu leo Tarehe 31/05/2020 amekutana na Bodaboda wa Wilaya ya Ikungi ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida kukutana na Makundi mbalimbali ili kupokea kero na changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi. #MtaturuJimboni

CHADEMA YAZIDI KUPUKUTIKA SINGIDA

Image
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida ndugu Shabani Limu Amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) rasmi leo 30/5/2020 nakukabidhi kadi ya chadema kwa Mhe. Munde Tambwe Abdallah (Mb)  Mjumbe wa Kamati kuu na mlezi wa CCM Mkoa Singida. #Ccm #Chaguolao

JENGO LA UPELELEZI KITUO CHA POLISI WILAYA YA IKUNGI KUKAMILIKA

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu leo 30/05/2020 amekabidhi mifuko ya Saruji ili nisaidie kumalizia Ujenzi wa Jengo la Upelelezi Kituo cha Polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida. #Mtaturukazini

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI YAENDELEA KUPATA HATI SAFI

Image
Mweyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally Juma Mwanga amewapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndugu Justice Lawrence Kijazi kwa kuendelea kusimamia ukusanyaji mapato na kuongeza Mapato katika Wilaya hiyo. #bazotvUpdate

ZIARA YA WAZIRI MEDARD KALEMANI SINGIDA MASHARIKI YALETA FARAJA KWA WANANCHI

Image
Baada ya Ziara ya Waziri Dkt Medard Kalemani Aprili 18, 2020 aliagiza Kijiji cha Kimbwi kuwekewa Umeme Ndani ya Siku 30 Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu Tarehe 17/05/2020 amefika kukagua mradi huo na nguzo 152 zimesimikwa, Wananchi wafurahia. #ManenokidogokaziZaidi #SindigaMasharikiMaendeleo

UTEKELEZAJI WA OMBI LA MBUNGE MTATURU WIZARA YA MAJI UNAENDELEA

Image
Baada ya mvua kusimama na Ardhi kuwa kavu hatimae Mkandarasi Target amefika Kijiji cha Sakaa kumalizia kuchimba kisima kirefu na Tarehe 17/05/2020 yamepatikana Maji Safi na baridi kwa Ajili ya Matumizi ya Wananchi, Vijiji vya Msuke, Mkunguwakihendo, Mampando, Msule na Ujaire vinafuatia. #ManenokidogokaziZaidi #SingidaMasharikiMaendeleo

MTATURU AWASILISHA KILIO CHA WASTAAFU:

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu amedai kuwa baadhi ya wastaafu wanashindwa kulipwa fedha zao kwa wakati na hivyo kuomba wasaidiwe kupata stahiki hizo kwani wametumikia vyema nchi hii. Mtaturu amesema hayo wakati akichangia mapitio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo ametolea mifano wa wazee wawili Gamaliel Mathia Masawe wa Makiungu na Mohammed Selemani Ntandu wa Unyahati wote wa jimboni kwake ambao hawajapata stahiki hizo kwa miezi saba.