Posts

Showing posts from October, 2019

SINGIDA: MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI MHE. MIRAJI MTATURU ATOA MILIONI 3 KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA ISSUNA - IKUNGI

Image
SINGIDA:  Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu Ametoa Shilingi Milioni tatu ili kuongezea Kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Issuna Wilayani Ikungi. Akiongea kwenye Mkutano na wananchi uliofanyika tarehe 02.11.2019 nje ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Issuna, amesema atahakikisha anapeleka kilio cha wananchi mahali husika ili wananchi waweze kupata huduma zote za afya katika maeneo yao. Aidha Mbunge Mtatutu amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuchagua viongozi waadilifu na watakao mpatia yeye ushirikiano wa kuwawakilisha wananchi na kutoa printer moja kwa ajili ya kuboresha huduma katika Shule ya Msingi Inang'ana Jimboni humo. 

GOOD NEWS: MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI MHE. MTATURU ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA MAPADRI KIBAONI SINGIDA

Image
Na bazil Mjungu: SINGIDA : Mbunge Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ameshiriki uzinduzi wa album ya Pili ya kwaya ya Bikra Maria Mama wa Mungu Parokia ya kibaoni Singida iliyopewa jina la Siri ya Mungu na Kuuza Cd na kufanikisha kupatikana kwa fedha zaidi ya Tsh milioni 4. Uzinduzi: Mtaturu akikabidhi CD alioizindua. Mhe. Mtaturu akimkadhi Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ikungi Ndg. Pius Sankha. Mbali na kiasi hicho cha fedha Mhe. Mtaturu alipata wasaa wa kutembelea jengo linaloendelea kujengwa watakalo ishi Mapadri na kujionea juhudi zilizofikia za ujenzi na kuamua kuchangia mifuko100 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya hiyo ya Mapadri. Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Mtaturu amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa kuwa na amani ili kuenzi amani tuliyo iachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. "Kwa hakika Tunaadhimisha miaka 20 tangu kufariki kwa muasisi wa Taifa letu aliyetuachia tunu ya amani, ni wajibu wetu sasa kuhakikisha tunail

NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA AKABIDHI MASHINE YA PHOTOCOPI SEKONDARI YA MANDEWA SINGIDA

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Musa Sima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Ametoa na kukabidhi Mashine ya kutolea kopi katika shule ya Sekondari Mandewa iliyopo Manispaa ya Singida Mkoni Singida, ikiwa ni katika kuhakikisha shughuli za uendeshaji wa shule hiyo haukwami, Akiongea kwenye Mahafali shuleni hapo Naibu Waziri Sima amesema, imefika wakati kila mtu kuelewa umuhimu wa Elimu na kutambua kua elimu haina mwisho hivyo wazazi, walezi na wadau wa Elimu kutosita kutoa ushirikiano katika kuendelea kufikisha huduma muhimu mashuleni. Akikabidhi Machine hiyo Mhe. Sima amewataka Wadau mbalimbali Nchini kufika maeneo walikosoma au kwenye Shule zenye changamoto na kuona ni jinsi gani kuweza kuzipunguza changamoto hizo na sio kusubiri tu serikali kwani serikali inapata taarifa kwa kuchelewa. Aidha, Mhe. Sima Amewataka wananchi wa Singida hususani ni wa Jimbo la Singida Mjini kushiriki kikamilifu shughuli za maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Mhe

WAZIRI MKUU MHE. KASIM MAJALIWA AFURAHISHWA NA SHUGHULI ZA KIWANDA CHA PAMBA CHA BIOSUSTAIN SINGIDA

Image
Na: Bazil Mjungu. SINGIDA : Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa ametembelea Kiwanda cha kusindika Pamba cha Biosustain kilichopo mjini Singida na kufurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho. Waziri Mkuu amefika na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo na kuonyesha kuridhishwa na Utendaji kazi wa kiwanda hicho. Waziri Mkuu KASIM MAJALIWA amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutumia dawa za asili ikiwemo ndulele na molases ili kuua wadudu waharibifu wa zao la pamba jambo ambalo limeongeza uzalishaji maradufu wa zao hilo. Waziri Mkuu pia amekitaka kiwanda hicho kununua Pamba kwa wakulima kwa bei nzuri ili kuinua kipato cha Mtanzania na kuhimiza  uongozi wa kiwanda cha Biosustain kuzingatia kulipa watumishi wao mishahara mizuri ili kuongeza morari ya kazi.      Akisoma taarifa fupi ya Kampuni hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Biosustain Tanzania Limited Dkt. Riyaz Haider amesema Kampuni ya Biosustain ilianza msimu wa uzalishaji wa Pamba mnamo mwaka 2006/20

MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI AMSHUKURU MAKAMU WA RAIS KWA KUTOA FEDHA KUKAMILISHA JENGO LA ZAHANATI ULYAMPITI

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu amemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  kwa kutoa Fedha kiasi cha shilingi milioni 154 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ulyampiti Wilayani Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki. Mbunge huyo amesema Makamu wa Rais alipofanya ziara ya kikazi hapo mwishoni mwa Mwaka 2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi yeye akiwa Mkuu wa Wilaya hiyo aliona ni jinsi gani wananchi wa Kijiji cha Ulyampiti wakitaabika kupata huduma za afya na kuamua Kumuomba mbele ya wananchi asaidie fedha za umaliziaji ujenzi wa Jengo la Zahanati hiyo ili kuweka karibu huduma ya Mama wajawazito, watoto wadogo na Wazee kuliko kufata huduma hiyo Ikungi, Itigi na Mkoani Singida. Akiongea na wananchi hao wa Kijiji cha Ulyampiti Mhe. Mtaturu amemshukuru Makamu wa Raisw Mhe. Samia Suluhu Hassani Pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa Kuwapatia wanan