Posts

Showing posts from September, 2019

MKUTANO WA MBUNGE SINGIDA MASHARIKI WAMNGOA MWENYEKITI CHADEMA

Image
IKUNGI: Mbunge wa Jimbo la  Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu leo 22.09.2019 amefanya mkutano na Wananchi Jimboni humo katika Kata ya Siuyu Wilayani Ikungi Singida ambapo Amefika kuwashukuru Wananchi kwa ushirikiano wao wanao utoa katika kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli za kufanya shughuli za maendeleo. Katika Mkutano huo alijitokeza aliyekua Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngaghe (CHADEMA) na kurudisha kadi ya chama hicho na kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM na kukabidhiwa kadi ya Chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu. Baada ya kupokea kadi ya CCM Aliyekua Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Ngaghe Ndg. Onesmo Kasmiri Msuta amesema ameamua kukihama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa kile alichodai amekaa miaka tisa (9) akiwa chadema na kukutana na Amri na Udikteta sio kanuni wala katiba za Chama kutoka kwa Aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu na kulazimishwa kuwaamuru Wananchi kutochangia wala kushiriki shughul

KISHINDO CHA MTATURU JIMBONI CHAZOA WAPINZANI 13

Image
Jumla ya viongozi na wanachama 13 wa vyama vya upinzani kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kutoka Cha Cha Wananchi (CUF) wamehama vyama vyao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kile walichodai kukubaliana na kasi ya Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuleta maendeleo. Miongoni mwa wanachama hao Katibu wa CUF Wilaya ya Ikungi Selemani Ntandu aliyekuwa katibu wa kuratibu shughuli za Lissu tangu 2007, mwenyekiti wa CHADEMA katika kijiji cha Ighuka Venance Elias na Katibu wa Chama hicho kata ya Ikungi Zakaria Kadagaa na Ezron Obed Kidumu -CHADEMA  Ikungi. Akikabidhi kadi kwa wanachama hao wapya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi Mhe. Mika Likapakapa amewataka wanachama hao kuwa waaminifu na watiifu kulingana na kiapo cha ahadi ya mwanachama na kutorudi nyuma katika kuhakikisha wanashiriki vyema kuendelea kukiimarisha chama . Akizungumza mmoja wa wanachama waliohamia CCM Selemani Ntandu amesema huo ni mwanzo tu lakini shughuli kama hiyo itaendelea. “ Mimi ndio niliku

MTATURU KUFADHILI WANAFUNZI 200 UNIFORM KILA MWAKA JIMBONI KWAKE

Image
Na Bazil Mjungu. IKUNGI : Wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi katika mkoa wa Singida wamejitokeza kwa wingi kumpokea Mbunge wao Mhe. Miraji Mtaturu aliyewasili akitokea Bungeni Jijini Dodoma baada ya kumaliza vikao vya Bunge. Mhe. Mtaturu amelakiwa na Wananchi wa Jimboni humo na kufanya mikutano kadhaa kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake. Mtaturu aliapishwa septemba 3 2019 Bungeni Dodoma baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Tundu Lissu (CHADEMA) kupoteza ubunge bada ya kukosa sifa kwa kutohudhuria vikao bila ya taarifa na kutojaza fomu za tamko la mali na madeni Bungeni. Akizungumza katika Mikutano aliyoifanya katika Vijiji vya Mkiwa, Issuna na Ikungi Mtaturu akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (MB) ameahidi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki wanapata maendeleo. Aidha katika mikutano hiyo ameweka bayana vipaumbele vyake atakavyovitekeleza katika kipindi cha Ubunge wake ambavyo ni Elimu

NAIBU WAZIRI TAMISEMI MWITA WAITARA AWASHUKIA WENYEVITI WASIO NA SIFA YA UONGOZI

Image
Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mwita Waitara (Mb), amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliomaliza muda wao ambao walikuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kashifa za migogoro hasa ya ardhi, wasijihangaishe kujuchukua fomu za kugombea nafasi hizo kwani muda waliokua madarakani hawakuweza kuwatumikia Wananchi ipasavyo. Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Waitara haliyasema hayo katika ziara yake ya kikazi katika Jimbo la Ukonga alipoenda kukagua miradi ya Maendeleo sambamba na kusikiliza kero za wananchi. "Nafasi yenu ya Wenyeviti wa Mtaa ni ya kujitolea  mlichaguliwa na wananchi ili muwatumikie muda wenu umekwisha wale Wenyeviti waliosababisha kesi za migogoro ya kuuza ardhi kiholewa na kutumia madaraka vibaya katika serikali ya amamu ya tano hawana sifa ya kuwa kiongozi majina yatakatwa"alisema Waitara.. Waitara aliwataka Viongozi wa chama wahakikishe wanapitisha majina ya watu wanaokubalika na jamii ili wapigiwe kura kwa ajili ya kuja kuongoz

Mkuu wa Wilaya Ikungi Edward Mpogolo Aanza ziara ya kikazi Kata kwa Kata

Image
MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Mhe Edward Mpogolo amefanya ziara yake ya kwanza ndani ya Wilaya hiyo toka ateuliwa na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli akichukua nafasi ya Mhe. Miraji Mtaturu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki. DC Mpogolo amefanya ziara katika Kata nne za Iyumbu, Mgungira, Ighombwe na Mtunduru ambapo alitembelea miradi ya Maendeleo, kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi pamoja na kueleza mambo makubwa ambayo yamefanywa na Serikali ya awamu ya tank chini ya Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli tangu apate ridhaa ya Wananchi kuiongoza Nchi kupitia CCM Mwaka 2015. Mhe. Mpogolo miongoni mwa kero ambazo amekutana nazo na kuzitolea ufafanuzi ni pamoja. Na changamoto ya maji, miundombinu ya barabara, uhaba wa vyumba vya madarasa, vituo vya afya, umeme na mawasiliano ambapo pia amewaeleza wananchi hatua ambazo Serikali imezichukua katika kuzitatua. "Ndugu zangu Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli kwa kutambua mnakabiliwa na changam

MTATURU NI SAHIHI SINGIDA MASHARIKI

Image
Na OMARY GWATY 0652162605 MH,MIRAJI MTATURU, Mbunge ingizo jipya la Singida Mashariki ni kiongozi anayeshughulika na shida za watu moja kwa moja,huyu hayupo kwenye Siasa za Maji taka,kwake fikra zake ni kuwapigania wananchi wake wapate Huduma zote wanazostahili! Hakuna jambo hata Moja ambalo huwa analifanya njee ya mipango. Kiufupi huyu kiongozi ana  Vission yake inayomwongoza.  Kiini cha Kazi zake ni kutengeneza mambo mapya, kuleta idea Mpya, Kufikiri katika Miaka zaidi ya Kumi Ijayo.  Utofauti wake mkubwa na viongozi waliopita ni kwamba hana Siasa za majigambo na matusi,chuki nk.huyu ni mstaarabu anayeamini katika Maendeleo kwa wote bila kujali itikadi ya chama,haya yalionekana akiwa DC wa Ikungi!   Tofauti nyingine ni kuwa wakati viongozi wengine walikuwa  wakiamka asubuhi wanafikiria ni wapi kwenye kero ya maji, Ardhi nk wakaweke maspika na kuanza kuhutubia kwa kudai kuwa wanasikiliza kero za wananchi....., MH MTATURU yeye huwa anatengeneza Mipango Mipya ya Utekelezaji, Swala la Ku