DAR es SALAAM: NUKUU ZA NDG. POLEPOLE KATIKA DARASA NA HIJJA YA KIITIKADI - TAWI LA CCM KATIKA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KIGAMBONI
Nukuu za Ngd Humphrey Polepole.
1. "Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilianzishwa na CCM tangu 1958 na hapa ndipo makada walipokuwa wanapikwa kiitikadi, ndio kilikuwa - Chuo Cha Kigamboni Cha Chama na tulipoanza mfumo wa Vyama vingi tukakitoa kwa Serikali bure, kuja hapa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni hijja ya kiitikadi kwetu" Ndg. Polepole
2. "Huwezi kuzungumzia historia ya Nchi yetu, ukakiacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani Chama chetu kina mahusiano ya moja kwa moja na historia ya Nchi yetu" Ndg. Polepole
3. "Maendeleo ni kitu kipana na kikubwa hivyo tuliopewa dhamana na mamlaka tunapaswa kuendelea na juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo kwa weledi maarifa na uaminifu mkubwa" Ndg. Polepole
4. "Mara nyingi baadhi yetu hatupendi kushukuru na kukubali ( appreciate) kwa mambo mazuri ambayo yanafanywa tena na watanzania wenzetu na tusipoweza kufanya hivyo hata kwenye mambo madogo kamwe hatuwezi kushukuru na kukubali (appreciation ) kwenye mambo makubwa" Ndg. Polepole
5. "Imani na Itikadi yoyote huwa vinakwenda sambamba na matendo na hakuna aibu kwenye Imani na Itikadi na ili tufanikiwe lazima tuwe wawazi sana kwenye Imani na Itikadi yetu" Ndg. Polepole
6. "Watu wanaopokea mawazo, maelekezo na maono ya Viongozi nawaomba muwe wabunifu wakati wa kuyaweka katika vitendo, tusiige tu bali tuyatafsiri katika namna njema" Ndg. Polepole
7. "Chama chetu ni cha kila mtu lakini ni lazima tuwafundishe wanachama, imani ya Chama chetu, masharti, sifa na ahadi za Mwanachama na umuhimu wa kuziishi" Ndg. Polepole
8." Kuwa mwanaCCM lazima uwe mnyenyekevu, mtulivu, mwenye kuheshimu watu, kufuata sheria, kanuni na taratibu za Chama chetu na nchi yetu" Ndg. Polepole
9. "Asili ya wanaCCM ni wachakarikaji sana, ni watafutaji sana na mali nyingi za CCM ni zao la wanaCCM wenyewe wamezitafuta wao, wale wanaosema kuhusu mali za CCM wafahamu hivyo" Ndg. Polepole
10. "Vijana msisubiri mpate hela ndio muwe na mawazo mazuri ya matumizi ya hela hizo, ni lazima muwe na mawazo mazuri kwanza kabla ya hela na mtafanikiwa, wakati wote hela hufuata mawazo mazuri" Ndg. Polepole
Katika Darasa hilo la Itikadi Ndg. Polepole ametoa kadi za uanachama wa CCM kwa wanaCCM wapya 456 kutoka katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere waliojiunga na CCM leo.
Imetolewa na,
*ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*
@bazilmj#
Comments
Post a Comment