Posts

Showing posts from April, 2023

MTATURU AITAKA SERIKALI KUJENGA SOKO LA KISASA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA IKUNGI

Image
na Bazil Mjungu: Dodoma MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itatenga fedha kwa ajili ya kujenga soko la kisasa wilayani Ikungi Mkoani Singida. Mtaturu ameuliza swali hilo April 24,2023, Bungeni Jijini Dodoma. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dr Festo Dugange amesema Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imeweka mpango wa kujenga soko la kisasa katika Kijiji cha Ikungi lenye ukubwa wa Ekari 2. Amesema kwa sasa Halmashauri inaendelea kufanya mazungumzo na wananchi ambao wamejenga vibanda vya biashara katika eneo hilo lililoainishwa na mipango miji kwa ujenzi wa soko la kisasa. "Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na UN WOMEN imekamilisha ujenzi wa jengo la mabucha na mbogamboga lenye thamani ya shilingi Milioni 82 katika eneo hilo,"amesema. Aidha, ameahidi kuwa serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa soko la kisasa Ikungi.

MILIONI 300 ZIMELETWA KUJENGA MABWENI SHULE YA MSINGI IKUNGI MCHANGANYIKO: MTATURU

Image
Na Mathias Canal, Ikungi-Singida Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha Miundombinu mbalimbali kwenye shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko ili kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji kwa watoto wenye mahitaji maalum ili kuweza kuongeza kiwango cha Elimu. Mbunge Mtaturu amesema hayo April 16, 2023 wakati akizungumza na watoto wenye mahitaji Maalumu baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa Bwalo la chakula, Mabweni Mawili ya Wasichana na Wavulana ambapo serikali ya Rais Dkt. Samia imepeleka fedha Shilingi Milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa miradi hiyo. Mtaturu aliihakikishia kamati ya shule pamoja na walimu wa shule hiyo kuwa kupitia ofisi yake ataendelea kutatua changamoto mbalimbali kwa makundi yenye uhitaji ili kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto hao. “ Nimshukuru Rais Samia ametuletea Milioni 300 kwaajili ya miradi ya ujenzi wa bw

TABASAMU LAONGEZEKA KWA WAKULIMA WILAYANI IKUNGI - SINGIDA

Image
Na Mwandishi wetu - Ikungi: Afisa Kilimo Ndugu Lucas Mkuki kutoka Sekretarieti ya Mkoa kwa niamba ya Katibu Tawala Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida awasisitiza wakulima kutumia mbinu za kisasa na kufuta kanuni bora za kilimo ili kufikia tija inayotakiwa katika kila mazao... Akizungumza katika Shehere ya Siku ya Mkulima Shambani iliyofanyika jana tarehe 06 April,2023 katika kijiji cha Matongo Meneja wa shirika hilo lisilo la kiserikali alisema wataendelea kufikia vijiji vingine na kutoa elimu hii lengo Ikiwa ni kukuza kilimo katika Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa singida kwa ujumla... Naye Afisa kilimo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo aliahidi kuendelea kufanya usimamizi wa hayo ili wakulima kuendelea kupata faida kubwa katika mradi huu wa Kilimo biashara "nitasimamia vikundi 40 ndani ya Wilaya yetu waliolima kwa tija ya kupata gunia 25 hadi 40 katika ekari 1" badala ya wakukima kulima kilimo cha mazoea.alisema Afisa Ki

ZIARA YA DC APSON, IKUNGI YAZIDI KUTATUA KERO, KUZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson amewataka wakandarasi kuzingatia ubora katika ujenzi wa miundombinu ya Serikali ili kuendana na wakati... Akizungumza mara baada ya kutembela Miradi mbalimbali leo tarehe 05 April 2023 ikiwemo shule ya Sekondari Mwau katika ujenzi wa maabara mbili za Kemia na biolojia zitakazogharimu Milioni 118.1,shule ya msingi Mwau katika ujenzi wa vyoo unalio fadhiliwa na Shanta Gold mine matundu 17 yaliyogharimu milion 46 pamoja na Zahanati ya Mang'onyi iliyogharimu Shilingi milioni 144.8 Mkuu wa Wilaya amewapongeza kwa hatua nzuri waliyoifikia na kushauri majengo yazingatie maagizo yanayotolewa na serikali... " Majengo lazima yawe yakisasa ili mtoto aweze kusoma katika mazingira yanayomvutia kuanzia sakafu,madirisha,rangi hata mabati yawe yakisasa ."alisema Mkuu huyo wa Wilaya ilaya... Kwa upande mwingine aliwapongeza Mgodi wa Shanta kwa kufadhili mradi wa vyoo pamoja na Zahanati ya Mang'onyi kwa kukamilika katika ubora na kuwaomba k