Na Bazil Mjungu Singida. Shirika la Restless Development Tanzania likiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bi. Haika, Meneja wa Miradi Bw. Ridhione Juma na Afisa mawasiliano wa shirika hilo wakiambatana na Saimon Sirilo Mratibu wa Vikundi vya Ujasiriamali kwa vijana Mkoa wa Singida. Wamewatembelea Vijana walionufaika na mafunzo ya Ujasiriamali yaliyotolewa na Shirika Hilo. Wilaya ya Ikungi na Itigi Mkoani humo Vijana wa Vikundi vya Ufugaji Nguruwe wa kisasa kutoka Mwisi, Kikundi cha Chaki kilichopo Mwisi, Kikundi cha Tofali Cha Puma na kikundi cha Tofali Ikungi. Vijana hao wamekiri kunufaika na mafunzo hayo na kusema mafunzo hayo yamewasaidia kufika mahali kwa kuanzisha Vikundi, kusajili na kupata Mikopo kutoka Halmashauri wanazo ishi. Aidha, Shirika limewasaidia Fedhaza chakula na usafiri uliowawezesha kushiriki kikamilifu mafunzo hayo. Uongozi wa shirika umewapongeza Viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata na Halmashauri kwa kushikamana na shirika hilo toka mwanzo hadi mwisho wa maf