MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA GEITA MHE. VICKY KAMATA AMEUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA RAIS MAGUFULI ZA TANZANIA YA VIWANDA KWA KUKABIDHI VITU VYENYE THAMANI YA MILIONI 125. MKOANI GEITA.
Na. Bazil Mjungu: Geita. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Mhe.Vicky Kamata ameunga mkono juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa Tanzania ya Viwanda kwa kutoa Vyerehani 350 kwa Kata zote za Mkoa wa Geita. Vyerehani hivyo vyenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 87.5 vimetolewa kwa Kata zote za Mkoa wa Geita. Pamoja na Vyerehani hivyo, Mbunge Vicky Kamata amekabidhi Shilingi Milioni 17.5 kwa ajili ya kutunisha Saccos za Akina Mama wa kata zote za mkoa wa Geita. Sambamba na hilo Mh. Vicky Kamata ametoa Chupa za Chai 360 kwa akina mama kwa ajili ya kuinua mitaji ya baadhi ya wamama lishe ili kusaidia kuinua vipato vyao. Akikabidhi vyerehani, fedha pamoja na chupa za chai kwa akina Mama hao Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabrieli amempongeza Mh. Vicky Kamata (Mb) kwa upendo aliounyesha kwa kina mama na kwa jamii ya wananchi wa Mkoa wa Geita kwa kuwajali wanawake na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuleta maendeleo. &q