Posts

Showing posts from December, 2020

MTATURU ATEMBELEA UJENZI WA SHULE YA MSINGI MBWANJIKI NA KUKABIDHI MIFUKO 30 YA SARUJI

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu leo 15/12/2020 Ametembelea ujenzi wa Shule ya Msingi Mbwanjiki na Kukabidhi Mifuko 30 ya Saruji. Mtaturu Amekabidhi Saruji hiyo baada ya Shule hiyo kukwama ujenzi wake kwa zaidi ya Miaka 30 iliyopita Shule hiyo ikikamilika itaondoa changamoto ya Wanafunzi kutembea umbali Mrefu na msongamano katika Shule wanazosoma za Ikungi, Ighuka na Matongo.

DIWANI PEKEE WA KATA YA NTUNTU AMBAYE NI MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA IKUNGI NA MJUMBE WA BARAZA KUU CHADEMA TAIFA ALA KIAPO CHA UDIWANI

Image
Diwani pekee wa Kata ya Ntuntu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ikungi na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Ndg. Omary Athumani Toto Ameapa mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ikungi kuwa Diwani wa Kata hiyo licha ya Halmashauri Kuu ya chama chake kuweka zuio la wanachama wote waliochaguliwa kutokula kiapo kwa kuwa chama hicho hakijakubaliana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu Mwaka 2020 na kuwa hawawatambui viongozi waliochaguliwa akiwepo Rais John Magufuli. Mhe. Omary Athumani Toto akipokea Ilani ya CCM kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt Rehema Nchimbi.

MTATURU ATOA MILIONI 1. UNUNUZI WA VYEREHANI VITANO CHUO CHA RYADHA CHA KIISLAM IKUNGI

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu leo 12/12/2020 Amehudhuria Kufungwa kwa Chuo Cha Kiislam Cha Ryadha Cha Ikungi Mkoani Singida na Kukabidhi Milioni 1 kwaajili ya Ununuzi wa Vyerehani vya kujifunzia Wanafunzi Chuoni hapo. #ManenoKidogoKazizaidi

MTATURU ATEKELEZA AHADI YA KUMPATIA BAISKELI MWALIMU ELIAS MKUKI (MLEMAVU) WA MUGHUMBU NTUNTU

Image
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Adam Mwiru Amemkabidhi Baiskeli Mwalimu wa kujitolea katika shule ya Msingi Mughumbu iliyopo Kata ya Ntuntu Mwl. Elias Mkuki ambaye ni Mlemavu wa Viungo ili imsaidie kufika Shuleni kwa wakati Baiskel hiyo imekua ni sehemu kutekeleza ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Miraji Mtaturu aliyowahi kuitoa kwake. Msaada huo ameutoa pia ili kuwaenzi watu wenye Ulemavu ambapo Disemba 03/2020 ilikuwa ni Maadhimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu Duniani. Akipokea Baiskel hiyo Mwl. Elias Mkuki amesema "Kwakweli nimejawana furaha kubwa mno Moyoni mwangu, aliniahidi siku zahivi karibuni kuwa ataniletea Baiskeli ninamshukuru nimeioata, Lakini niseme tu kwamba kuna viongozi wengi huwa wana ahidi Wananchi na hata walemavu Kama Mimi lakini hawatekelezi kwakweli Mungu amlinde Mtaturu katika Utumishi wake" alisema Mwl. Elias. #bazotvNewsUpdate.