MVUA YASABABISHA UHARIBIFU WA MASHAMBA YA KAYA 93 RORYA MARA
Na_Bazil Mjungu. ROYRA MARA : Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyo nyeesha Desemba 12/2019 katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilayani Rorya Mkoani Mara imesababisha maporomoko makubwa ya mawe na mmomonyoko mkubwa wa ardhi hali iliyopelekea kuharibika kwa mashamba ya Kaya zaidi ya 93. Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo (CCM) alitembelea eneo hilo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Charles Ochele na viongozi wengine wa Serikali za Vijiji na Kata kufika katika eneo la tukio na ujionea uharibifu mkubwa Mashamba kusombwa na Maji yenye Mawe Makubwa yaliyosababisha kutokea kwa mto na bonde kubwa huku za zaidi ekari 20 za mazao ya wananchi kusombwa na maji na kuharibiwa na mamia ya mawe yaliyoporomoka kutoka zaidi ya km 2 kutoka eneo la Mashamba n Mlima uliko. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Tatwe Mhe. Lameck Airo ametoa pole kwa wananchi na kuonyesha kusikitishwa na tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi na kuwashitua wananchi