MTATURU AIOMBA SERIKALI KUANZISHA MAMLAKA YA MAJI MJI WA IKUNGI
Na Bazil Mjungu: Dodoma MBUNGE wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ametaja mambo manne ya kuzingatiwa katika kuhakikisha hali ya upatikanaji maji katika wilaya ya Ikungi inakuwa ya kuimarika ikiwemo kuhakikisha vijiji kumi vinapata chanzo cha maji cha uhakika. Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji Mei 7 bungeni ametaja vijiji hivyo kuwa ni Ntuntu, Taru, Mbogho, Mwau, Mahambe, Choda, Manjaru, Tumaini, Matongo na Unyakhanya. “Nikupongeze Waziri na timu yako kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuhakikisha wananchi wanapata maji,na Ilani yetu ya Uchaguzi ya CCM katika ukurasa wa saba Ibara 9 D kifungu cha kwanza imeeleza wazi katika miaka mitano kuwa itaongeza nguvu katika upatikanaji wa maji, “Hivyo katika hili kasi inatakiwa iendelee kuongezeka katika kuwekeza zaidi, najua kazi imefanyika na mimi nina ushahidi katika jimbo langu au Wilaya ya Ikungi tumepata bilioni 3.7 kwa mwaka uliopita,safari hii naona wametubana sana kwa wilaya nzima tumepata Bilioni 1.7 ,maa