Posts

Showing posts from July, 2020

MTATURU ASHIRIKI UJENZI WA UPANUZI WA IKULU CHAMWINO - DODOMA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu leo tarehe 12/07/2029 ameshiriki Ujenzi wa Upanuzi wa Ikulu ya Chamwino - Dodoma.

MTATURU AMEFIKA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUMUONA MGONJWA ALIYE MSAFIRISHA KUTOKA KIPUMBWIKO KUJA KUTIBIWA HAPO NA YEYE KUGHARAMIA MATIBABU YAKE

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu amefika Hospital ya Benjamini Mkapa kumuona Mgonjwa Bi. Elizabeth Lissu aliyemsafirisha kutoka Kipumbwiko Ikungi kuja kupatiwa matibabu baada ya Mbunge kujulishwa kuwa Mama huyo amepooza miguu na yupo kitandani zaidi ya Mwaka bila kupatiwa matibabu. Mhe. Mtaturu amekubali kugharimia Matibabu ya bi Elizabeth Lissu na madaktari wameeleza atafanyiwa kipimo cha MRI.

VIJANA 52 KUTOKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA WAHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI IKUNGI

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Ndg. Mika Likapakapa amepokea  Vijana 52 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA walioamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa kile walichodai kuwa wamechoshwa na tabia za chama hicho za kuwalazimisha kuwakataa hata wazazi wao kisa wako CCM, Vijana hao wamedai kufurahishwa na Utendaji kazi za Maendeleo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi kifupi cha Miezi 9 tangu kuapishwa Bungeni September 3/2019.

Mhe. MTATURU NA TISA YA UTUMISHI.

Image
Na Koti la Kung'aa. Brazili ni nchi pekee duniani iliyowahi kuishikilia historia ya soka la dunia kwa muda mrefu sana na vijana wengi walikuwa wanatamani kupata fursa ya kumiliki hata chembe ya uwezo wa aliyekuwa mmoja wa Icon ya soka la Brazil kati ya Carlos Dunga na kina Ronaldo De Lima katika kulisakata Samba (Soka la Kibrazili) Kitu pekee kilichowahi kumbeba Ronaldo De Lima, nguli huyu aliyekabidhiwa jezi nambari 9 ni ufundi,ubunifu na matumizi ya maarifa ya ziada katika kuhakikisha timu inapata matokeo yenye furaha kwa wabrazili na wafuasi wa soka la Brazili. Hoja yangu sio soka la Brazili na wababe wake bali ni * UBUNIFU ,MAARIFA,USHAWISHI NA UFUNDI * katika jimbo la Singida mashariki ambalo mpaka makala hii inaenda kwenye tanakilishi lilikuwa linaongozwa na Mheshimiwa Miraji J. Mtaturu aliyetumia miezi tisa tu kupambana na changamoto za wananchi kupitia nafasi yake kama mbunge. Kimahesabu Mheshimiwa Mtaturu amekaa ofisini (Kama mbunge)kwa sekunde 388800 ambazo ni sawa